logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Na hii sura yangu nzuri yenye urembo uliopitiliza siwezi sikiliza miziki ya gengetone - Gloria Ntazola

Alisema kwamba kumtaka asikilize gengetone ni sawasawa na kumlazimisha kula nyama ya nguruwe.

image
na Davis Ojiambo

Burudani03 January 2024 - 08:07

Muhtasari


  • • Ntazola safari hii amerudi na kusisima vita dhidi ya miziki ya Gengetone akisema kwamba hata kwa mtutu wa bunduki hawezi jipata anasikiliza miziki hiyo.
  • • Alisema kwamba kumtaka asikilize gengetone ni sawasawa na kumlazimisha kula nyama ya nguruwe.
Gloria Ntazola.

Gloria Ntazola, mrembo na mjasiriamali wa vipodozi aliyepata umaarufu wa ghafla mwaka jana baada ya kupapurana na askari wa kaunti ya Nairobi – Kanjo, amerudi tena mwaka huu kwa vishindo vya aina yake.

Ntazola safari hii amerudi na kusisima vita dhidi ya miziki ya Gengetone akisema kwamba hata kwa mtutu wa bunduki hawezi jipata anasikiliza miziki hiyo.

Mrenbo huyo akitoa sababu yake kwa uamuzi huo, alisema kwamba kwanza miziki ya gengetone haina ujumbe maana ya kusikilizwa Zaidi ya kelele tu za ala za muziki na pili urembo wake ni wa kupindukia ambao hauwezi kumpa nafasi ya kusikiliza miziki kama hiyo.

“Huwa sisikilizi miziki ya Kenya kwa sababu hakuna cha mno cha kusikilizwa mle. Na huu urembo wangu eti nijipate nasikiliza gengetone? Jamani hapana! Wasanii wenyewe ni wazembe ambao hawana hata uwezo wa kuwekeza katika Sanaa yao, heri tu tujikite katika riadha,” Ntazola alisema.

 Lakini pia, Ntazola alisema kwamba ukimtaka kufanya chaguo kati ya gengetone na miziki ya kutoka Magharibi mwa Kenya, yeye atachagua miziki ya Kiluhya pasi na kupepesa jicho.

Alisema kwamba kumtaka asikilize gengetone ni sawasawa na kumlazimisha kula nyama ya nguruwe, kitu ambacho anakichukia mno.

“Heri nisikilize nyimbo za Waluhya kuliko nikae nikisikiliza Gengetone. Kuniambia nisikilize genetone ni sawa na kunishrutisha nikule nyama ya nguruwe, kusema ukweli sipendi huyo mnyama hata kidogo,” Ntazola aling’aka.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved