Manzi wa Kibera amtema mpenziwe wa miaka 66 baada ya kupata mpya wa miaka 75

“Nimepata new catch, huyu sasa ndio nimechagua 2024, na natumai mtamkubali na mmkaribishe pia. Na nimeridhika." Manzi wa Kibera alisema.

Muhtasari

• Lakini kilichowashangaza wengi ni kwamba Manzi Wa Kibera tena amerudia pale pale, kwani mpenzi wake mpya tena ni mzee, safari hii mwenye miaka 75.

Manzi wa Kibera na mpenzi mpya.
Manzi wa Kibera na mpenzi mpya.
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Manzi wa Kibera kwa mara nyingine yuko kwenye vichwa vya habari baada ya kuanza mwaka 2024 na joto jingine tofauti.

 Mrembo huyo anayejitapa kuwa anatokea kaika mtaa wa mabanda wa Kibera ameanza mwaka na mpenzi mpya, baada ya kudokeza kumuacha aliyekuwa mpenzi wake kwa kipindi cha mwaka mmoja, mzee mwenye umri wa miaka 66.

Lakini kilichowashangaza wengi ni kwamba Manzi Wa Kibera tena amerudia pale pale, kwani mpenzi wake mpya tena ni mzee, safari hii mwenye miaka 75.

Akimtambulisha kwa mashabiki wake kupitia blogu ya Nocholas Kioko, Manzi wa Kibera alisema kwamba yeye ana nyota ya wazee, akisema kwamba ana uwezo mkubwa wa kuwa’handle watu wazima wenye umri umesinyaa.

“Nimepata new catch, huyu sasa ndio nimechagua 2024, na natumai mtamkubali na mmkaribishe pia. Na nimeridhika. Niko na damu ya wazee kwa sababu nahisi najua kuwadhibiti. Wazee ndio zangu, nadundadunda tu hapo kwa wazee,” Manzi wa Kibera alisema.

Akijitambulisha, mzee huyo alisema jina lake ni Daniel Njau na kuahidi kukwama katika penzi la Manzi wa Kibera hadi pale ambapo Mungu ataridhia.

“Naitwa Daniel Njau, ndio. Nafikiri maisha ni yetu mimi na wewe mpaka wakati Mungu mwenyewe atakapoamua, si umeridhika na mimi?” Mzee huyo alimuuliza Manzi wa Kibera.

Mrembo huyo amemtambulisha mpenzi mpya miezi michache tu baada ya kuzua taarifa mpya mitandaoni kwamba alikuwa na ujauzito wa aliyekuwa mpenzi wake, mzee wa miaka 66.

Ama kweli ukistaajabu ya musa na firauni, utayaona na Manzi wa Kibera na wazee wake.