logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bwana mkunaji naomba uje unifunze jinsi ya kukuna kuna - Stevo Simple Boy (video)

Huu mwaka wa 2024 nataka kukuna kuna kunakuna - Stevo alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani10 January 2024 - 07:34

Muhtasari


  • • Hata hiovyo, kwenye upande wa kutoa maoni, baadhi ya watu walihisi alikuwa anamchokoza msanii Willy Paul ambaye katika siku za nyuma alikuwa anajitambulisha kwa msimbo ‘Bwana Mkunaji’.
Stevo Simle Boy

Msanii Stevo Simple Boy amezua utani mitandaoni baada ya kuomba kupewa mafunzo jinsi ya kukuna.

Katika Instagram yake, alipakia video akiomba jamaa anayejiita ‘Bwana Mkunaji’ kumfuata ili kumpa mafunzo ya kukuna kwa sababu lengo lake kuu katika mwaka wa 2024 ni kujua jinsi ya kukuna.

“Kuna mtu anajiita bwana mkunaji, mimi kama Stevo Simple Boy naomba aje anifunze jinsi ya kukuna kuna. Huu mwaka wa 2024 nataka kukuna kuna kunakuna. Tafadhali, njoo bwana mkunaji unifunze jinsi ya kukuna kuna, au sio, ndio maanake,” Stevo Simple Boy alisema.

Hata hiovyo, kwenye upande wa kutoa maoni, baadhi ya watu walihisi alikuwa anamchokoza msanii Willy Paul ambaye katika siku za nyuma alikuwa anajitambulisha kwa msimbo ‘Bwana Mkunaji’.

Hata hivyo, Pozee baadae mwaka jana alidondosha msimbo huo akisema kwamba asingependa tena kuendelea kutambuliwa na mashabiki hivyo kutokana na dhana mbaya ambayo ilikuwa imeanza kuhusishwa na msimbo huo.

“Utagongwa na pozee ww” Salma Abdallah.

“willy Paul onyesha uyu kukuna” Pracydea.

“@willy.paul.msafi Habari do hiyo” Ricks Musyio.

Hii inakuja siku chache baada ya msanii huyo kudai kwamba angependa kurejelea katika miziki ya injili baada ya kupungwa na wimbo wa Bunny Asila na Christina Shusho.

 Hata hivyo, hajaonekana kutii neno lake kwani hivi majuzi tena alionekana kujiingiza katika uanaharakati baada ya kudokeza kionjo cha wimbo wake wa kiharakati kuhusu baa la njaa na jinsi serikali imekuwa ikiwakandamiza walala hoi.

“Wakenya kweli twateseka watoto wanalala bila chakula, bei kweli imepanda hata za vyakula, sasa imekuwa tabu kula, serikali imekwepa kutupa mahindi, watu wachomeka kwa duka la wahindi, Wakenya mbona tusiwe washindi…” sehemu ya mistari ya wimbo huo wa kiharakati iliimba.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved