Katika miaka ijayo Obinna atafikia viwango kama vya Steve Harvey - Ezekiel Mutua atabiri

“Ninajitolea kumshauri na kumuombea ukuaji wa kazi mwaka huu. Oga umebarikiwa. Nenda mbele na ushinde ulimwengu!” Mutua alimwambia Obinna.

Muhtasari

• Mutua alitoa utabiri kwam ba Obinna ana kila kinachohitajika kuwa kama host wa vipindi vya runingani wa Marekani Steve Harvey.

Ezekiel Mutua na Oga Obinna
Ezekiel Mutua na Oga Obinna
Image: Facebook

Afisa mkuu mtendaji wa MCSK, Ezekiel Mutua ametoa utabiri wake wa kiuhakika kumhusu mchekeshaji ambaye pia ni YouTuber Oga Obinna.

Mutua kupitia Facebook yake alipakia msururu wa picha ambazo walipigwa na Obinna wote wakiwa wamevalia nadhifu.

Mutua alitoa utabiri kwam ba Obinna ana kila kinachohitajika kuwa kama host wa vipindi vya runingani wa Marekani Steve Harvey.

Alisema kuwa hilo halina shaka kwani katika miaka kadhaa ijayo, Obinna atakuwa ndiye Steve Harvey wa Kenya kwa jinsi anavyojitutumua katika mitikasi yake kwenye ukuzaji maudhui haswa kweney kipindi chake cha ‘Obinna Show’ kinachokwenda mbashara kwenye YouTube kila wiki.

“Katika miaka ijayo, Oga Obinna atapanda hadi viwango vya Steve Harvey katika afya na utajiri na athari ya kimataifa katika kazi yake,” Mutua alitoa utabiri wake.

Mutua ambaye pia anajulikana kwa misimamo yake thabiti dhidi ya mienendo ya kupotosha kijamii na pia mlokole wa kupigiwa mfano alisema ameamua kujitoka kumpa hamasa Obinna lakini pia kumuombea ili kuhakikisha utabiri huo wake juu yake unatimia.

“Ninajitolea kumshauri na kumuombea ukuaji wa kazi mwaka huu. Oga umebarikiwa. Nenda mbele na ushinde ulimwengu!” Mutua alimwambia Obinna.

Wanamitandao walimhongera Mutua kwa kujitolea kumpa ushauri Obinna jinsi ya kujiendeleza Zaidi ili kufikia viwango vya mastaa wa kimataifa kama Harvey na wengine.