'Kuna kuna' ya Vic West na 'Enjoy' ya Jux kati ya ngoma 10 anazopenda Lupita Nyong'o 2024

Wimbo wa Kuna KUna ulitolewa mwezi Oktoba mwaka 2022 na ukaibuka kuwa wimbo pendwa na vijana wenye umri wa makamo.

Muhtasari

• Hivi majuzi, muigizaji huyo aligonga vichwa vya habari baada ya kupakia video akila msosi wa ajabu wakati wa ziara yake nchini Benin.

• Lupita katika video hiyo alikuwa akila kwa mara ya kwanza nyama ya nyoka aina ya Viper.

Lupita Nyong'o
Lupita Nyong'o
Image: Facebook

Muigizaji wa Kenya anayeishi Mexico, Lupita Nyong’o ametoa orodha ya nyimbo 10 bora ambazo angependelea kuzisikiliza Zaidi mwaka wa 2024.

Kupitia Instagram yake, Lupita Nyong’o alipakia orodha ya ngoma 10 pendwa kwa mwaka 2024 na kwa bahati nzuri kati ya ngoma hizo 10, mbili ni za kutoka Afrika Mashariki.

Mshindi huyo wa tuzo za Oscar mwaka 2014 aliorodhesha ngoma ya Kuna Kuna ya msanii Vic West akiwashirikisha wasanii wa Gengetone kama Brandy Maina, Fathermoh, Thee Exit band na Savara kama wimbo wa Kikenya ambao unampunga sana na angependa kuusikiliza tena mwaka 2024.

Pia katika orodha hiyo alitaja wimbo wa Enjoy wake Juma Jux akimshirikisha Diamond Platnumz kutoka Tanzania, ukiwa katika nafasi ya 7.

Nyimbo nyingine ambazo Lupita aliorodhesha ni pamoja na;

This Year wa Emily King

Good Morning wa PJ Morton

It’s So Easy wa Margo & Mac

Deggi Gui wa Cheikh Lo

Next to Normal wa Lucius

Nueva Vida wa Peso Pluma

By Design [Evel Knievel] na Jacob Banks

Doing my Best na Tank and The Bangas

Hivi majuzi, muigizaji huyo aligonga vichwa vya habari baada ya kupakia video akila msosi wa ajabu wakati wa ziara yake nchini Benin.

Lupita katika video hiyo alikuwa akila kwa mara ya kwanza nyama ya nyoka aina ya Viper.

Baada ya kuonja kwa woga mwingi, muigizaji huyo alionekana kufurahia akisema kwamba nyama ya nyoka kwa asilimia kubwa ladha yake inawiana na ya kuku.