Bobrisky atangaza rate card yake ya 2024, "Kunisalimia tu unalipa Ksh 319k"

Bobrisky ni mtumbuizaji wa mitandaoni kutoka Nigeria ambaye anavaa mavazi ya kike baada ya kujibadilisha jinsia yake kutoka mwanamume kupitia msururu wa upasuaji.

Muhtasari

• Mtu huyo wa mtandaoni alisisitiza kwamba yeyote anayevutiwa na ofa zake atalazimika kuzungumza na meneja wake.

Bobrisky
Bobrisky
Image: Instagram

Mwanasosholaiti mwenye utata kutoka Nigeria, Bobriksy ameibuka na bei mpya za huduma zake mbalimbali kwa mwaka huu wa 2024.

Bobrisky ambaye anatajwa kuwa mwanamume aliyejibadilisha jinsi na kuwa mwanamke aghalabu anajulikana na wengi kama mwanamume anayejivika mavazi ya kike.

Akitangaza ‘rate card’ yake mpya, Bobrisky alisema kwamba mwaka huu mambo ni tofauti kwani lazima aendelee kuongeza urembo na uzuri na hawezi kuacha fursa yoyote ya kutengeneza pesa kumponyoka.

Kilichowashangaza wengi, Bobrisky katika rate card yake alisema mpaka kukutana naye kwa salamu tu ni pesa ndefu ambazo mtu atahitajika kutoka huku akisema baadae atakuja kuachia bei ya yeyote anayetaka kumuoa.

Bobrisky, ambaye hivi majuzi alikuwa amefanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti (Augmentation mammoplasty), alitumia ukurasa wake wa Instagram, akisema bei yake imeongezeka.

Aliandika, "Bei za mummy wa Lagos ziliongezeka. Kusema tu "hi" kwa mummy wa lagos $2,000, Unataka kumkumbatia mummy wa lagos $5,000, Unataka mummy wa lagos kukubusu shavuni  $10,000, Muda mfupi na mummy wa lagos $100,000, Usiku mzima mummy wa lagos $300,000, na bado sijatoa bei ya kumuoa mummy wa Lagos."

Mtu huyo wa mtandaoni alisisitiza kwamba yeyote anayevutiwa na ofa zake atalazimika kuzungumza na meneja wake.

Aliandika, “Utahitaji kuzungumza na meneja wangu @ladygolfer001 ili akupe risiti. 2024 ashewo pro max”.