Nandy ashinda shindano la kumtungia Haji Manara wimbo, akabidhiwa hundi 50m

“Tulifanya challenge na tukampata mshindi. Ningetamani sana mshindi awe msanii wa kuchipukia lakini mimi nilikuwa natafuta mshindi halali wa wimbo utakaonivutia mimi,” Manara alisema.

Muhtasari

• “Nandy ndio mshindi, tulikuwa tunataka kufanya kama katafrija hivi na ndio maana tuko hapa kumkabidho hundi,” Manara aliongeza.

Nandy na Manara.
Nandy na Manara.
Image: Scree ngrab

Hatimaye shindano la Haji Manara kumtafuta msanii aliyemtungia wimbo uliomfurahisha limekamilika na mshindi kupatikana.

Siku chache zilizopita, Manara alitangaza ofa kwa msanii yeyote ambaye atamtungia wimbo wa kumsifia na mpenzi wake mpya, Zaylissa.

Akitangaza mshindi jioni ya Alhamisi, Manara aliema kuwa alikuwa anamtafuta msanii aliyetunga wimbo wa kumfurahisha, na kwa bahati nzuri msanii Nandy ndiye aliyeibuka mzuri kwa wimbo uliomfurahisha tajiri Manara.

“Tulifanya challenge na tukampata mshindi. Ningetamani sana mshindi awe msanii wa kuchipukia lakini mimi nilikuwa natafuta mshindi halali wa wimbo utakaonivutia mimi,” Manara alisema huku akitetea uamuzi wa kuikubali ngoma ya Nandy.

“Nandy ndio mshindi, tulikuwa tunataka kufanya kama katafrija hivi na ndio maana tuko hapa kumkabidho hundi,” Manara aliongeza.

Msemaji huyo wa zamani wa timu ya soka ya Yanga SC alimpa Nandy zawadi ya hundi ya shilingi milioni 50 pesa za Kitanzania kwa kuibuka mshindi kwenye challenge hiyo.

Uvumi wa Manara kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Zaylissa, muigizaji ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa msanii Dulla Makabila, ulianza mwishoni mwa mwaka jana baada ya penzi lake la awali na wanawake wawili kusambaratika kwa njia tofauti.