Mcheza santuri wa kike maarufu nchini, DJ Pierra Makena amekanusha kupitia mzozo wa kinyumbani na babydaddy wake kupelekea yeye kuonekana na maumivu mwilini.
Hii ni baada ya kupakia video akionekana kuwa na uvimbe sehemu za uso na kuwaambia mashabiki wake kuwa alikuwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake walihisi kwamba uvimbe huo huenda ulisababishwa na kichapo kutoka kwa baba wa mtoto wake ambaye waliachana akiwa na mimba ya miezi mitano na ambaye hajawahi muonesha mitandaoni.
Lakini baada ya uvumi huo kuenezwa, Makena alirudi mitandaoni na kunyoosha maelezo akisema kwamba hakupigwa bali ni ugonjwa tu na kuwataka mashabiki wake kupunguza kasi ya mashambulizi kama hayo.
"Fam mimi ni bora sasa na kupata matibabu kutoka nyumbani. Sikupigwa hivyo jeshi langu lishushe silaha zao. Nilipata athari ya mzio kutoka na maumivu makali ya chini ya mgongo. Maelezo ya mzio nikipata nafuu. Asante kwa kufikia na kuwa huko. Nawapenda nyote,” alisema.
Pia alikanusha uvumi kwamba alipata ajali ya barabarani kupelekea uvimbe huo na kuwashukuru mashabiki wake kwa kusimama upande wake muda wote kutaka kujua kilichomdhuru.
“Hapana sikupigwa wala sikupata ajali ya gari. Yote yako chini ya udhibiti na shukrani kwa hati na wauguzi ambao walinihudumia haraka huko ER. Napata nafuu kutoka nyumbani kwa mapumziko ya kulazimishwa / ninayostahiki.. muwe na wiki yenye baraka familia,” Makena alisema.