Drake afurahia babake kurudi nyumbai baada ya miaka 15 na kujumuika na familia

Kwa mujibu wa HotNewHipHop, mamake Drake, Sandi amekuwa akiishi Toronto, Kanada, huku babake, Dennis akimlea msanii huyo huko Memphis, Tennessee, Marekani.

Muhtasari

• Akiwa anachukua kwenye Instagram story yake usiku wa kuamkia leo, Drizzy alifichua kuwa babake Dennis sasa ameruhusiwa kurudi Canada.

• Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo kumsaidia mtu kuweza kusafiri kwa uhuru.

•  Drizzy, kama anavyojiita, alimsaidia msanii 21 Savage kupata Green Card ambayo hatimaye ilimruhusu kuingia Kanada.

DRAKE
DRAKE
Image: Instagram

Rapa kutoka Kanada, Drake ni mwenye furaha baada ya babake hatimaye kupewa kibali cha kurudi nchini mwao – Kanada baada ya Zaidi ya miaka 15.

Kwa miaka mingi, Drake amekuwa akiwazungumzia wazazi wake kwa njia sawa kwenye mitandao ya kijamii, licha ya wote kutenganishwa kimazingira kwa muda huo wote.

Kwa mujibu wa HotNewHipHop, mamake Drake, Sandi amekuwa akiishi Toronto, Kanada, huku babake, Dennis akimlea msanii huyo huko Memphis, Tennessee, Marekani.

“Kwa miaka mingi, Dennis hajaruhusiwa nchini Kanada kutokana na masuala fulani ya kisheria. Hii ina maana kwamba megastar huyo wa HipHop ameweza tu kumuona baba yake wakati akisafiri kwenda Marekani,” ripoti hiyo ilisoma.

Akiwa anachukua kwenye Instagram story yake usiku wa kuamkia leo, Drizzy alifichua kuwa babake Dennis sasa ameruhusiwa kurudi Canada.

Kwa kweli, Dennis alisherehekea kwa kuungana tena na ex wake Sandi. Wawili hao walionekana wakiwa na tabasamu kwenye nyuso zao.

"Kwa Mara ya kwanza katika zaidi ya miaka 15 waliruhusu OG kurudi Canada," Drake aliandika. "Asante kwa kila mtu aliyetusaidia."

drake
drake

Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo kumsaidia mtu kuweza kusafiri kwa uhuru. Drizzy, kama anavyojiita, alimsaidia msanii 21 Savage kupata Green Card ambayo hatimaye ilimruhusu kuingia Kanada.

Wawili hao walikuwa kwenye tour pamoja, na rapper huyo alihitaji Green Card ili kufanikisha ziara za Kanada.