Nabii kutoka Ghana amtaka Wizkid kuwa makini na watu wanaomzunguka, ataja kifo (video)

“Taarifa hizi zitakuwa kubwa, zitazua mtetemeko katika tasnia ya muziki wa sekula Nigeria. Na kwako tena, omba sana ili kilichotokea kwa Davido kisije kikatokea kwako,” nabii huyo alihubiri.

Muhtasari

• "Nyoka huyu atakuuma wakati mwafaka ukifika kama hutakuwa makini,” nabii huyo alihubiri.

WIZKID
WIZKID
Image: Facebook//WIZKID

Video inayomuonyesha mchungaji mmoja kutoka nchini Ghana akitabiri kitakachokuwa chanzo cha kifo cha msanii wa Afrobeats kutoka Nigeria, Wizkid imezua tumbojoto katika mtandao wa blogu ndogo ndogo wa X.

Katika video hiyo iliyopakiwa na mtumizi mmoja kwa jina Olomide, mchungaji huyo kutoka Ghana anayejitambulisha kama nabii alisikika akimtahadharisha kwa sauti ya kuogofya msanii Wizkid na kumtaka kuwa makini na watu anaokaa nao.

Kwa mujibu wa nabii huyo, Wizkid atamalizwa na kusafirishwa jongomeo na rafiki yake wa karibu ambaye anajifanya kuwa karibu naye kumbe ni adui yake.

“Wizkid! Kuna nyoka mkubwa anayekuzingira, nyoka huyo amejituliza lakini atakuuma wakati mwafaka ukifika. Hii itakuwa habari kubwa katika historia ya muziki wa Nigeria. Kuna nyoka anayemzingira Wizkid, anajiweka kirafiki sana kwake, kwa sasa hana madhara yoyote kwake. Nyoka huyu atakuuma wakati mwafaka ukifika kama hutakuwa makini,” nabii huyo alihubiri.

Pia alimtahadharisha kuwa makini Zaidi na nyendo zake ili yasije kumkuta kama yale yaliyomkuta mwenzake, Davido.

 Itakumbukwa mwaka juzi, Davido alifiwa na mwanawe Ifeanyi katika tukio la kutatanisha baada ya kudaiwa kuzama nyumbani kwenye bwawa la kuogelea.

Taarifa hizo ziligonga vichwa vya habari kote duniani, huku kukiibuka dhana tofauti tofauti zilizohusishwa kifo cha mrithi huyo wa pekee wa Davido.

“Taarifa hizi zitakuwa kubwa, zitazua mtetemeko katika tasnia ya muziki wa sekula Nigeria. Na kwako tena, omba sana ili kilichotokea kwa Davido kisije kikatokea kwako,” nabii huyo alihubiri.

Itakumbukwa Wizkid na Davido wamekuwa wakishindana kwa Zaidi ya muongo mmoja kwenye malimwengu ya muziki wa Afrobeats, kila mmoja akijishindia tuzo kivyake kiasi kwamba mashabiki mitandaoni wamegawanyika kwa pande mbili kila mmoja akisepa na kijiji chake cha mashabiki utadhani ni mashabiki wa timu za mpira.

Nchini Nigeria, kwa sasa wawili hao wanajulikana kama ‘The Big 2’ lakini miaka ya hivi majuzi pia msanii Burna Boy amejiunga kwenye kundi lao na kuitwa ‘The Big 3’

Wizkid alifiwa na mamake mzazi mwaka jana, tukio ambalo alisema lilimpokonya furaha yake wakati ambapo alikuwa anaihitaji Zaidi.