Ombi la Stevo Simple Boy ni kukutana na Jalang'oo ili wale chips kuku pamoja

“Mheshimiwa unaweza tengeneza siku moja tukutane, tukale chips kuku, ama hamburger ama kitu kama ugali hivi, tafutasiku tukutane,” Stevo alisema.

Muhtasari

• Kwa upande mwingine, alipoulizwa kama anaweza kufanya kolabo na KRG, Stevo alisema kwa msisitizo kwamba KRG si msanii bali ni vixen.

Stevo Simple Boy
Stevo Simple Boy
Image: Screengrab

Rapa Stevo Simple Boy ameomba kukutana na mbunge wa Lang’ata Jalang’oo kwa ajili ya kushereheka mlo mtamu pamoja, siku chache tu baada na mbunge huyo kumsifia pakubwa.

Stevo katika mazungumzo na YouTuber Trudy Kitui, alisema kwamba anashukuru Jalang’oo kumkubali kuwa kwa sasa hakuna rapa anayemzidi na kusema kwamba ombi lake ni kukutana na mbunge huyo siku moja ili wakasherehekee mlo wa chips kuku au hata ugali.

“Mheshimiwa unaweza tengeneza siku moja tukutane, tukale chips kuku, ama hamburger ama kitu kama ugali hivi, tafutasiku tukutane,” Stevo alisema.

Hii inakuja siku chache baada ya Jalang’oo kusema kwamba msanii yeye ni shabiki mkubwa wa msanii huyo tangu 2019 alipotoka na wimbo wa midaharati.

Jalang’oo alisema kwamba hata juzi alimpigia simu Stevo wakati wa kuvuja kwa video ambapo alikataa kumpa salamu aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy.

Mbunge huyo ambaye amewahi kuwa mchekeshaji, msanii na mtangazaji kwenye redio alisema kwamba alimshauri Stevo kwa njia ya simu kutokataa kumsalimia Ex wake kwani kwa wakati mmoja aliwahi kuwa mtu wa kumpa furaha.

Kwa upande mwingine, alipoulizwa kama anaweza kufanya kolabo na KRG, Stevo alisema kwa msisitizo kwamba KRG si msanii bali ni vixen tu wa kuonekana kwenye kazi za Sanaa.

“KRG si msanii, yeye ni vixen tu. Hata kama unafanya kolabo na msanii kutoka Jamaika, mimi sijali, wewe ni vixen, tafuta siku moja uje ukuwe kama vixen kwenye muziki wangu,” Stevo alisema.