logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Usiweke ukali kunakohitajika wema na upendo' - Mammito amsihi Sonko kuhusu Conjestina

“Ugonjwa wa akili ni mkali na huchukua muda kwa mtu kupona kabisa" Mammito alisema.

image
na Radio Jambo

Habari17 January 2024 - 06:06

Muhtasari


• Sonko alisema kwamba Conjestina alilazimika kurudi kwa watu wake baada ya kile alisema ni kuwepo kwa muingiliano kutoka kwa watu wa karibu.

Mammito amsihi Sonko kuwa mpole kwa Conjestina

Mchekeshaji Mammito Eunice ametofautiana kauli na mhisani Mike Sonko baada ya kuandika kwamba anampa aliyekuwa bondia mashuhuri nchini Conjestina Achieng nafasi ya mwisho katika majaribio mengi ya kujaribu kumsadia kimatibabu.

Mammito kupitia ukurasa wake wa X alinukuu chapisho la Sonko ambapo alisema kwamba hii itakuwa mara yake ya tatu na ya mwisho kwa Conjestina Achieng kujaribu kumpeleka kaitka kituo cha kurekebisha tabia ili kupata suluhu la tatizo la akili ambalo limekuwa likimsumbua kwa miaka mingi sasa.

Mammito alimshauri Sonko kutokuwa mkali anapojaribu kumsaidia Conjestina, kwani mpaka kukubali kurudi katika kituo cha kurekebisha tabia kwa ajili ya matibabu ya tatizo la akili, tayari hiyo ni hatua kubwa ambaye Conjestina amefanikisha.

Alimtaka kuwa mpole anaposhughulikia kisa kama cha Conjestina kwani ni mgonjwa tu wa tatizo la akili, akisema kwamba matatizo ya kiakili si jambo dogo kama ambavyo wengi wanalichukulia.

“Ugonjwa wa akili ni mkali na huchukua muda kwa mtu kupona kabisa… ni mchakato na huwezi kuweka kikomo wakati mtu atapona kabisa. Utayari wake wa kwenda kwenye rehab ni hatua, kwa hivyo uwe mkarimu. Wacha apone kwa kasi yake mwenyewe! Usiwe mkali ambapo wema na upendo unahitajika,” Mammito Eunice alimshauri Sonko.

Awali, tuliripoti kwamba Sonko alikuwa amekubali kumrudisha Conjestina rehab katika kile alikitajak uwa ni ‘kwa mara ya tatu na mwisho’ ikiwa tayari amejaribu kumhudumia hapo awali lakini juhudi zake zikaja kuonekana kutozaa matunda dakika za mwisho.

Mwaka jana baada ya kufanikisha kupona kwa bondia huyo wa zamani, Sonko alimpa kazi kama mmoja wa walinzi wake lakini mapema Janauri ikabainika kwamba Conjestina amerejelea hali yake za zamani akiwa mgonjwa nyumbani kwa mama yake, Yala kaunti ya Siaya.

Hili lilizua mfarakano mkali mitandaoni Wakenya wakimnyooshea Sonko mtutu wa bunduki na kumlazimu kuelezea kinagaubaga kilichotokea hadi Conjestina akaacha kazi ya ubaunsa kwake na kurudi nyumbani kwa mamake akiwa katika hali mbaya.

Sonko alisema kwamba Conjestina alilazimika kurudi kwa watu wake baada ya kile alisema ni kuwepo kwa muingiliano kutoka kwa watu wa karibu.

Lakini safari hii tena ameamua kumrudisha katika chuo cha rehab kuona kama juhudi zake kwa mara ya mwisho zitazaa matunda ili bondia huyo arejeee hali yake za zamani akiwa mzima na buheri wa afya.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved