Meneja wa Diamond, Sallam SK avunja kimya kuchomeka kwa studio za redio yake

“Kila jambo hutokea kwa kheri yake, kwa niaba ya @mjinifm nataka nitoe shukurani kwa wote waliotufarariji tulipopata matatizo ya kuunguliwa na studio zetu," SK alisema.

Muhtasari

• “Kila jambo hutokea kwa kheri yake, kwa niaba ya @mjinifm nataka nitoe shukurani kwa wote waliotufarariji tulipopata matatizo ya kuunguliwa na studio zetu," SK alisema.

SALLAM SK
SALLAM SK
Image: INSTAGRAM

Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam SK ambaye pia ni mfanyibiashara na mmiliki wa kituo cha redio amevunja kimya chake takribani wiki mbili baada ya moto kuchoma studio za stesheni yake ya radio, Mjini FM.

SK kupitia ukurasa wake wa Instagram alipakia picha za masazo ya studio hiyo na kusema kwamba kila kitu hutokea kwa mipango ya Mungu lakini kaitka hilo, aliumia pakubwa.

Mjasiriamali huyo aliwashukuru wote waliosimama na familia nzima ya Mjini FM wakati wa kisa cha moto na kusema kwamba wao ni mashabiki wa maana sana.

Alifichua kwamba kituo hicho cha redio kimesharejea hewani na kazi inaendelea kama kawaida.

Kila jambo hutokea kwa kheri yake, kwa niaba ya @mjinifm nataka nitoe shukurani kwa wote waliotufarariji tulipopata matatizo ya kuunguliwa na studio zetu, nitoe shukurani kwa zima moto, mkuu wa kituo cha polisi Oysterbay, Tanesco na wote waliohusika kufika kwa wakati pale janga lilipotokea. Endelea kusikiliza 92.5 MJINI FM ipo hewani kama kawaida na KAZI IENDELEE 🙏🏽” SK alichapisha.

Baadhi ya mashabiki wake kwenye chapisho hilo walizidi kumfariji wakisema kwamba kila kitu kitajipa tu na kuendelea kama kilivyopangwa na Mungu.

“Pole boss tuko pamoja” Zuchu alimwambia.

“Poleni Salam na team nzima ya mjini fm.Mungu awatangulie” Joseph Kusaga alisema.

“Pole sana,” Mkubwa Fella alisema.