Mrembo mtangazaji afungua paybill kuchangiwa pesa za mazishi ya paka wake wa kiume

“Hata sitaki pesa nyingi, nataka shilingi 20 tu kutoka kwa kila mtu ili nipange mazishi… nitashukuru sana, nyinyi wote ni watu wangwana sana,” Githinji aliandika.

Muhtasari

• Mashabiki wake katika mtandao huo walijibu instastory hiyo wakimtaka kuweka namba ya kutuma michango kwa ajili ya mazishi ya paka Mimi.

Natalia Githinii afiwa na paka
Natalia Githinii afiwa na paka
Image: Instagram

Mrembo Natalia Githinji ambaye ni mtangazaji katika kituo kimoja cha redio za mjini humu nchini anaomboleza kifo cha paka wake wa kiume kwa jina Mimi.

Githinji kupitia uurasa wake wa Instagram Story, alichapisha bango la kuomboleza kifo cha ghafla ya mnyama huyo pendwa akisema kwamba alikuwa amesalia na mwezi mmoja tu kumaliza miaka miwili tangu alipokutana naye kwa mara ya kwanza.

“Kwa ajili ya kumbukumbu ya upendo ya Mimi, Nilimkuta mara ya kwanza Februari mosi 2022 lakini amefariki Januari 17 mwaka 2024, mtoto wetu mpendwa,” Githinji alindika kwenye bango hilo.

kifo cha paka
kifo cha paka

Mashabiki wake katika mtandao huo walijibu instastory hiyo wakimtaka kuweka namba ya kutuma michango kwa ajili ya mazishi ya paka Mimi.

Githinji aliwajibu akisema kwamba hakuwa anataka pesa nyingi bali alitaka tu shilingi 20 kutoka kwa kila mmoja mwenye kuguswa ili kuandaa mazishi ya kufaa kwa paka wake mpendwa.

“Hata sitaki pesa nyingi, nataka shilingi 20 tu kutoka kwa kila mtu ili nipange mazishi… nitashukuru sana, nyinyi wote ni watu wangwana sana,” Githinji aliandika.

Wengine wakidhani ni mchezo, Bi Githinji alienda mbele na kuchapisha paybill kwa ajili ya miamala hiyo akisema kwamba angependa kumheshimu paka wake hadi pale anapoelekea mchangani.

“Mnaweza tuma meseji kwa DM yangu lakini msitume kitu chochote Zaidi ya shilingi 20. RIP mpenzi wangu Mimi, hii ni ya wale ambao waliitisha Paybill,” aliandika huku akifichua Paybill hiyo ambayo sisi hatuna idhini na mamlaka ya kuichapisha hapa.

"R.I.P Mimi, nakupenda vibaya sana mahn. Alikuwa daima kwa ajili yangu hasa baada ya upasuaji wangu na wakati endometriosis ilikua inaniweza .... wanyama ni uaminifu bora, wanastahili kila kitu. Naomba Mimi aende mbinguni 😇 😇" aliongeza.