Aliyekuwa msanii chini ya lebo ya Konde Music Worldwide, Anjella amefichua orodha ya watu maarufu ambao wamemlisha block kwenye mtandao wa Instagram.
Anjella alikuwa anajibu shabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu na jibu hilo lake kuhusu watu maarufu ambao wamemblock lilinakiliwa na blogi moja kabla ya kuyeyuka baada ya saa 24.
Anjella aliwashangaza mashabiki wake kwa kufichua kwamba miongoni mwa watu maarufu ambao hawezi kuzungumza nao kwa vile wamekwishamblock ni watu waliokuwa maswahiba wake katika lebo hiyo inayomilikiwa na Harmonize.
Alisema kwamba Harmonize, Kajala na bintiye Paula wote wamemblock.
“Mtu gani maarufu amekublock?” aliulizwa.
“Konde, Kajala na Paula,” Anjella alijibu.
Hata hivyo, mashabiki wengi walionekana kumshambulia kwa kile walisema kwamba tangu aondoke katika lebo hiyo, amekuwa akifunguka mambo mengi sana kuhusu mabaya ya lebo yenyewe, wakimtuhumu kwa kukosa fadhila.
Haya hapa ni baadhi ya maoni ya watu walioona chapisho hilo;
“Hapo kwa konde She deserves it 😒she’s so ungrateful 🙄” Arlene Bad Girl alisema.
“Umeongea ujinga weee bado unataka mtu asikublock?” Carlosjoachim.
“Bora tu una mdomo sana mtu mwenyewe tulikujua kupitia konde,” suleimanaziza.
“Sikapendi sikuhizi haka kadada” abaya pambee.
“Mdomo ulimponza” celestinapaulo.
“Hamornize kumblock hajakosea mtu anapokutendea wemaa kuwa na shukran kwa machache hayo bila harm tusingemjuaa huyu bintiii” lightnessmonyo.
“KONDE HATAKAGI UJINGA YANI AMEKUSAIDIA ALAFU BADO UNAONGEA VITU VYA AJABU NJE STUPID KABISA” BizzybrownTz.