"Niliumia sana kwa kweli kusikia KRG ameniita kilema" - Stevo Simple Boy afunguka

“Kwa kweli iliniuma sana, lakini nilijua tu haya ni mambo tu ya majibizano, tuone ubabe wa kila mtu. Siwezi jua ni kitu gani kilimfanya KRG kuniita kilema, siwezi jua,” Stevo alisema.

Muhtasari

• KRG kwa dharau alisema kwamba hana tamko lolote la kumjibu Stevo, akimtaja kuwa ni kilema.

Stevo na KRG
Stevo na KRG
Image: Facebook

Rapa Stevo Simple Boy amefunguka kwa mara ya kwanza hisia zake baada ya msanii KRGtheDon kumuita kilema.

KRG katika mahojiano kwenye kituo kimoja cha redio humu nchini katika ziara ya kupigia debe kolabo yake na Konshens, aliulizwa kuhusu Stevo kumtaja kuwa si msanii bali ni vixen wa kwenye video.

KRG kwa dharau alisema kwamba hana tamko lolote la kumjibu Stevo, akimtaja kuwa ni kilema.

Sasa Stevo baada ya kuulizwa hilo katika blogu moja ya Trudy Kitui, alifunguka kwamba tamko hilo la KRG lilimuumiza sana lakini akasema kwamba haliwezi kumtikiza kwa njia yoyote kwani amezoea kubandikwa majina hasi.

“Kwa kweli iliniuma sana, lakini nilijua tu haya ni mambo tu ya majibizano, tuone ubabe wa kila mtu. Siwezi jua ni kitu gani kilimfanya KRG kuniita kilema, siwezi jua,” Stevo alisema.

Hata hivyo, msanii huyo alisema kwamba tamko hilo la KRG licha ya kwamba linaonekana kumnyanyapaa na kumdhalilisha, halikuonekana kuwa na uzito wa kiasi hicho kwa familia na watu wake wa karibu.

Stevo alisema kwamba ana mke ambaye ni muelewa wa ajabu na familia yake pia ambayo inajua kwamba tamko hilo lilikuwa ni tu miongoni mwa maneno ya kutupiana mradi kulichangamsha genge.

“Mke wangu anaelewa, na pia familia yangu inaelewa, walisema tu kwamba haya ni maneno tu ya kimuziki,” Stevo aliwatoa wasiwasi mashabiki wake waliomkasirikia KRG.