Kumekucha kulichele katika ndoa ya msanii Mr Seed na mpenziwe, Nimo Gachuiri!
Mr Seed amejipata katika sehemu mbaya baada ya matamshi yake kuhusu wanaume kuwa na asilia ya kuoa wanawake wengi kumuudhi mpenzi wake Nimo.
Msanii huyo alitokea kwenye podcast moja na kuzungumzia mambo ya mahusiano na akasema msimamo wake kwamba kwa tajriba yake kwenye ndoa, mwanamume ni kiumbe ambaye anaweza akawa kwenye ndoa na mwanamke kwa miaka 3 lakini bado akawa anawazia kuoa mwanamke mwingine.
Seed alisema kwamba wanaume kwa kawaida ni wa mitala na kwamba mwanamke kuishi na yeye kwa muda mrefu si kigezo cha kumfanya kuhisi kwamba ameshinda, kwani anaweza amka siku moja tu agundue mume wake anapanga kufunga harusi na mwanamke mwingine hali ya kuwa yeye bado yupo.
“Hebu niambie, sisi wanaume tuna akili. Ninaweza kuwa na wewe kwenye uhusiano kwa miaka kama 3 unaelewa? Miaka mitatu tu ya mimi kukutazama nikijua vizuri huna ninachokitaka.”
“Kwa hivyo niko hapo halafu siku moja unaamka na kukuta jamaa tayari ameshaandaa harusi kwa sababu msichana huyu tayari alidhani alikuwa mshindi. Tuna marafiki wengine wa kike sawa? Miongoni mwa marafiki hao, tunaangalia kati yao kuona nani ni mke mzuri. Labda hata ni rafiki yako mkubwa,” Mr Seed alisema kwa kujiamini. "Wanaume wamecreatiwa kuwa na wake wengi."
Matamshi haya yalionekana kumuudhi mno mkewe Nimo ambaye kupitia Instastory yake alimkanda vikali akisema kwamba matamshi kama hayo hayafai kutoka kwa kinywa cha mwanaume anayejua kwamba yuko katika ndoa imara.
"Kwa hivyo niliona kipande kidogo cha podikasti iliyofanywa na Mr Seed, akisema chochote alichokuwa akisema. Hata sikumaliza kuitazama. Nilikasirika. Basi nikamgeukia na kumuuliza, hizi sasa ni nini unasema hakika. Kitu kingine nilichosema lazima watu wafikiri mimi ni mjinga! Kwa hivyo alikuwa kama unapaswa kutazama podikasti nzima na walichagua sehemu hiyo pekee ili iweze ku-trend,” aliandika kwenye hadithi zake za Insta.
"Ninachotaka kusema ni kama ni kwa ajili ya mapenzi, lilikuwa jambo lisilo na hisia kusema wakati uko katika uhusiano wa kujitolea," alisema zaidi.
Kwa tathmini ya haraka, Nimo alikuwa tayari ameshakatisha urafiki kwa mumewe katika mtandao wa Instagram.
Hata hivyo, kuangalia katika ukurasa wa mumewe, Mr Seed, yeye bado alikuwa hajakatisha urafiki wake kwani bado anam’follow Nimo.