Mulamwah afichua kiasi cha pesa alitumia kukodisha farasi kwa ajili ya babyshower

Huyu atakuwa mtoto wao wa kwanza pamoja, lakini wa pili kwa Mulamwah ambaye tayari ni baba kwa bintiye muigizaji Carrol Sonie.

Muhtasari

• Kupitia instastory yake, Mulamwah alieleza kwamba farasi hao kukodishwa kwa kila saa ni shilingi elfu 50.

Mulamwah.
Mulamwah.
Image: Facebook

Mchekeshaji Mulamwah amefichua kiasi cha pesa alizogharamika kukodisha farasi kwa ajili ya babyshower ya mpenzi wake Ruth K.

Kupitia instastory yake, Mulamwah alieleza kwamba farasi hao kukodishwa kwa kila saa ni shilingi elfu 50 na muda wa chini kabisa wa kuwakodisha ni saa 4, kwa maana kwamba huenda alitumia shilingi laki mbili kufanikisha shughuli hiyo.

“Kwa wale mnaouliza, farasi ni shilingi elfu 50 kwa kila sana muda wa chini kuwakodisha ni saa 4,” Mulamwah alifichua.

mulamwah
mulamwah

Mulamwah na Ruth K waliandaa sherehe ya babyshower kwa ajili ya mwanao mtarajiwa wikendi iliyopita katika hafla ambayo alionekana kwenye video ‘akimnyeshea mvua ya pesa’ mpenzi wake.

Wiki chache zilizopita, Mulamwah na Ruth K walifichua jinsia ya mwanao – wa kiume – katika video nzuri ambayo waliigiza kama watafiti kwenye maabara.

Huyu atakuwa mtoto wao wa kwanza pamoja, lakini wa pili kwa Mulamwah ambaye tayari ni baba kwa bintiye muigizaji Carrol Sonie.

Hata hivyo, baada ya kuchapisha picha hizo, baadhi ya mashabiki wake katika mitandao ya kijamii walianza kumtania kwamba farasi hao ndio wale waliombeba Akothee na aliyekuwa mpenziwe Mr Omosh Aprili mwaka jana wakati wa harusi yake.

Itakumbukwa Akothee na Omosh waliachana miezi michache tu baada ya harusi ya kifahari iliyohakiniza kwenye vichwa vya habari kote nchini.