Burna Boy aondoka stejini kwa hasira baada ya mitambo ya sauti kufeli akitumbuiza (video)

Burna pia alisikika akiiambia timu yake kwamba hajawahi kuhisi aibu hiyo hapo awali katika maisha yake.

Muhtasari

• Vipaza sauti vyake vilikuwa vimewashwa hivyo alikuwa akisikia tu kucheza na hakutambua hadi baada ya muda.

• Mara tu Burna Boy alipogundua hilo, aliondoka jukwaani ili kuwa na mazungumzo makali na waandaji wa hafla hiyo.

Burna Boy
Burna Boy
Image: Facebook

Msanii atakayetumbuiza katika hafla ya kutolewa tuzo za Grammy wa 2024, Burna Boy alionekana kwenye video akiondoka jukwaani wakati wa onyesho nchini Ivory Coast baada ya kipaza sauti chake kutofanya kazi.

Katika video iliyotumwa mtandaoni, Burna Boy alionekana akijaribu kuwatumbuizia umati wa watu kwenye tamasha moja nchini Ivory Coast bila kujua kuwa mtambo wa sauti ulikuwa umefeli na sauti yake kutoka kwa kipaza sauti haikuwa inasikika kwenye spika.

Vipaza sauti vyake vilikuwa vimewashwa hivyo alikuwa akisikia tu kucheza na hakutambua hadi baada ya muda.

Mara tu Burna Boy alipogundua hilo, aliondoka jukwaani ili kuwa na mazungumzo makali na waandaji wa hafla hiyo.

Hakurudi kumaliza yake na alisikika akiwafokea watu wake kwamba walete gari karibu ili aweze kuondoka katika sehemu hiyo.

Hata hivyo, kuondoka kwake kwa hasira pia hakukuchangiwa na kufeli kwa mtambo wa sauti bali pia kulisikika baadhi ya mashabiki wakimpigia kelele kwa kulitaja jina la Davido – mpinzani wake katika muziki wa Afrobeats.

Burna pia alisikika akiiambia timu yake kwamba hajawahi kuhisi aibu hiyo hapo awali katika maisha yake.

Tamasha hilo lililofeli siku chache baada ya onyesho la kwanza la Burna Boy mjini Abidjan, ambapo aliwaenzi magwiji wengi wa soka barani Afrika, wakiwemo Emmanuel Adebayor na Jay Jay Okocha.

Hivi majuzi alifungamana na Tems kama msanii wa Nigeria aliyeingiza nyimbo 100 zaidi za Billboard Hot.

Pamoja na kushirikishwa kwenye orodha ya nyimbo anazopenda za mwaka za Barack Obama.

Ziara yake ya Amerika Kaskazini 'I Told Them' itaendelea Februari hii, 2024