Haji Manara ampokonya mke na kudaiwa kumpleka polisi msanii wa Singeli, Dulla Makabila

Manara alipeleka uhusiano wake mpya na Ex wa Makabila kwa kuandaa bonge la sherehe ya kumvisha pete wikendi iliyopita.

Muhtasari

• Makabila katika utunzi wake, alimrejelea Manara kama ‘Mzungu’ kutokana na ulemavu wake wa ngozi kwa maana kwamba yeye ni zeruzeru.

Zaylissa abadilisha wing'i kutoka kwa Makabila kwenda kwa Manara.
Zaylissa abadilisha wing'i kutoka kwa Makabila kwenda kwa Manara.
Image: Facebook, Instagram

Unaambiwa cheza utakavyo lakini usicheze na watu wenye pesa zao!

Tajiri Haji Manara baada ya kumpokonya mke msanii wa singeli, Dulla Makabila, ameongeza msumari moto kwenye kidonda kwa kudaiwa kumshtaki polisi kisa kumchamba kwamba amemchukulia mke.

Zogo lilianza pale ambapo msanii Dulla Makabila alipokosana na mpenzi wake, muigizaji Zaylissa ambaye hakukawia sokoni kwani alikwapuliwa na Haji Manara.

Manara alipeleka uhusiano wake mpya na Ex wa Makabila kwa kuandaa bonge la sherehe ya kumvisha pete wikendi iliyopita.

Hili lilionekana kuwa pigo kubwa kwa Makabila ambaye kwa uchungu aliingia studioni na kuwatungia wimbo akimuapiza Manara na Zaylissa kwa viwango sawa.

Makabila katika utunzi wake, alimrejelea Manara kama ‘Mzungu’ kutokana na ulemavu wake wa ngozi kwa maana kwamba yeye ni zeruzeru.

Pia alimkaripia Zaylissa akimtaja kama mwanamke aliyefuata pesa na si mapenzi ya kweli, na kufichua kwamba alikuwa ananywea P2 ili asipate mimba yake.

Makabila alimtaka Ex wake kumzalia ‘mzungu’ na pia kumpiga kumbo kwenye kitovu akisema kwamba hajui kupika.

Maneno haya ya shombo kwenye wimbo wa Makabila hayakuonekana kukaa sawa kwa Manara ambaye anasemekana kupiga ripoti polisi akitaka kijana huyo kuadhibiwa.

Jumatano Makabila alielekea kituoni kuitikia wito baada ya kukabidhiwa barua kwamba anatakikana kufika kituoni.

“Mimi nimeitwa, nimeambiwa kwamba nina kosa la matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, kwa hiyo tumeyazungumza na kuzungumzika na nimepewa tarehe ya kuja kuripoti tena. Nilivyoambiwa ni kuhusiana na wimbo ule kama unaonekana unaleta shinda,” Makabila alisema.

Hata hivyo, wakili wake alikanusha kwamba si Manara aliyepeleka taarifa polisi bali ni polisi tu walimtaka kwenda kupiga ripoti kuhusu zogo linalondelea kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini kwa wale wanaofuatilia zogo hilo kwa ukaribu wanaamini kabisa kwamba taarifa hizo kufika katika kituo cha polisi, kuna mkono wa Manara nyuma yake.