Kusema kweli sikuwa najua mzee alikuwa anauza vitu vyake kunihudumia - Manzi wa Kibera

Akiulizwa ni nini atafanya kumsaidia mzee huyo kumkwamua kutoka kwa maisha duni baada ya kula bata na yeye hadi kumkausha, Manzi wa Kibera alisema;“Nitasimama na yeye tu kwa maombi tu."

Muhtasari

• Pia alimtumia vijembe mzee huyo kwa kudai kwamba alikuwa anatongoza wasichana wengine kipindi wako pamoja lakini akamsikitikia kwa hali aliyokuwa nayo sasa.

MANZI WA KIBERA
MANZI WA KIBERA
Image: instagram

Manzi wa Kibera kwa mara ya kwanza ameonysha kuhuzunika na hali halisi ya aliyekuwa mpenzi wake, mzee wa miaka 66.

Katika mahojiano na YouTuber Nicholas Kioko, Manzi wa Kibera alijuta kwa jinsi mzee huyo anavyochakura makapi na kusema kwamba ukweli wake ni kuwa hakuwahi jua kwamba mzee huyo alikuwa anauza vitu vyake vya nyumba ili kumhudumia enz wakiwa wapenzi.

Mzee huyo baada ya kuonekana katika hali ya kutamausha kwenye mtaa duni wa Kibera, alisema kwamba Manzi wa Kibera alimkwepa baada ya kula vya kwake na sasa amebaki banu wala sakanu.

Pia alimtumia vijembe mzee huyo kwa kudai kwamba alikuwa anatongoza wasichana wengine kipindi wako pamoja lakini akamsikitikia kwa hali aliyokuwa nayo sasa.

“Ninamhuzunikia sana mzee na kwa wakati huu wenye dhoruba, nasimama na yeye. Lakini zile DM alikuwa anajibu, nimeshangaa, nilidhani atapata mrembo mwingine, lakini kama ameamua kuja kulia na nafikiri alitoka kwangu na kifua kizito, nini kingine naweza sema, namsikitikia tu,” Manzi wa Kibera alisema.

“Kusema ukweli mimi sikuwa najua kwamba mzee alikuwa anauza vitu vyake kunihudumia, na ninamsikitikia, ninamuombea mazuri, yaani hata sina kitu cha kusema, ninahisi vibaya na hizo stori, lakini kwa wakati huo huo niko na furaha na mpenzi wangu mpya hapa,” aliongeza.

Akiulizwa ni nini atafanya kumsaidia mzee huyo kumkwamua kutoka kwa maisha duni ambayo amejipata nayo baada ya kula bata na yeye hadi kumkausha, Manzi wa Kibera alisema;

“Nitasimama na yeye tu kwa maombi. Nitamsapoti kimaombi tu, na kama ni pesa pengine ni elfu 5 hivi tu, tutaona.”

Mzee wake mpya alimuunga mkono katika hilo na kusema amempa ruhusa ya kwenda kumfariji ex wake.

“Sasa wewe chenye utafanya, wewe tuliza roho yake, usimuonyeshe ubaya wowote, iwe tu kwamba mko pamoja japokuwa mumetengana kidogo. Na kama atakuwa na shida yoyote tafadhali msaidie,” mzee huyo wa miaka 75 alimshauri.