Kama msichana niliyekua bila baba sitaki kuona binti yangu akikua bila baba - Georgina Njenga

“Na kama binti ambaye nilikua bila kumuona babangu, siwezi taka kuona mtoto wangu akikua bila baba yake,” aliongeza.

Muhtasari

• Alisema jambo moja linalomfanya kutomzuia Baha kujenga uhusiano wake na binti yao ni kwamab alikulia maisha ya bila upendo wa baba.

Mpenzi wa zamani wa muigizaji Tyler Mbaya maarufu kama Baha Machachari
Georgina Njenga// Mpenzi wa zamani wa muigizaji Tyler Mbaya maarufu kama Baha Machachari
Image: Screengrab//YouTube

TikToker Georgina Njenga amefunguka kuhusu malezi ya binti yake Astra, hasa baada ya kuachana na babydaddy wake, Tyler Mbaya maarufu kama Baha Machachari.

Akizungumza na Nicholas Kioko, Njenga alimtetea mpenzi huyo wake wa zamani na kufichua kwamba kwa muda ambao wamekuwa kila mtu akiishi kivyake tangu Julai mwaka jana, Baha amekuwa akijaribu kadri ya uwezo wake kukaa karibu na binti yao.

Georgina Njenga alisema kwamba hawezi katu kumzuia Baha kumuona binti yake kwani hata atuame vipi hawezi badilisha ukweli kwamba huyo ndiye baba kwa binti yao Astra.

 Alisema jambo moja linalomfanya kutomzuia Baha kujenga uhusiano wake na binti yao ni kwamab alikulia maisha ya bila upendo wa baba, kitu ambacho hatokubali kije kutokea katika maisha ya binti yake.

“Ni kweli tunashirikiana kulea mtoto wetu asilimia 100. Yeye atabakia kuwa baba kwa binti yangu na siwezi pata mbadala wake hata nifanye nini. Anatoa matunzo, wanaonana, ako pale katika maisha ya binti yetu 100%,” Georgina Njenga alisema.

“Na kama binti ambaye nilikua bila kumuona babangu, siwezi taka kuona mtoto wangu akikua bila baba yake,” aliongeza.

Mrembo huyo mama wa mtoto mmoja alisema kwamba ili kuhakikisha binti yake hapitii maisha ya kukosa upendo wa baba kama yeye, anahakikisha kila kitu anampa kipaumbele Zaidi Astra katika kila jambo.

“Mara moja unapoelekeza fikira zako kwamba mtoto wangu ndiye anakuja wa kwanza, hakuna kitu kitakachokubadili katika hilo. Tunashirikiana katika malezi kwa ajili yake, kwa hiyo yeye ndiye huja wa kwanza katika picha.”

Georgina alisema kwamba katika maisha Yake, amekuja kukubali kwamba Astra hana boma moja la kuita nyumbani bali ni mtoto wa pande mbili – kwa baba na kwa mama – na hilo ndilo limefanya uhusiano wao kuendelea bila doa licha ya kwamba kwa sasa kila mmoja anajishughulisha na maisha yake kivyake.