Megan Thee Stallion aongeza ulinzi kwa kaburi la mamake ugomvi na Nicki Minaj ukizidi kutokota

Mzozo wa Nicki na Megan ulianza Ijumaa wiki jana pale Nicki alipofanya wimbo na ndani yake kumuimbia Megan akimwambia "Afadhali uende kumpa ujauzito mama yako na kuomba msamaha."

Muhtasari

• Mama yake Megan Thee Stallion, Holly Pete, alizikwa, baada ya kufariki mwaka 2019 kutokana na saratani ya ubongo.

• Mzozo huo ulianza Ijumaa baada ya Nicki kufanya kile ambacho wengi wamekiita mzaha usiofaa kuhusu mamake Megan kwenye jukwaa la utiririshaji la Stationhead.

//Megan Thee Stallion aongeza ulinzi katika kaburi la mamake
BIFU ZITO //Megan Thee Stallion aongeza ulinzi katika kaburi la mamake
Image: Facebook

Msanii Megan Thee Stallion kutoka Marekani amesemekana kuongeza ulinzi katika la marehemu mama yake huku ugomvi wake na rapa mwenza Nicki Minaj ukichukua mkondo tofauti, TMZ inaripoti.

Mashabiki wa Nicki Minaj, walitinga eneo la makaburi ambapo mama yake Megan Thee Stallion, Holly Pete, alizikwa, baada ya kufariki mwaka 2019 kutokana na saratani ya ubongo, chombo cha habari kinaripoti.

Baadhi ya mashabiki hao walivujisha lokesheni hiyo na kuwahimiza wengine kulichafua kaburi la mama huyo baada ya Megan kudaiwa kuichana familia ya Nicki katika wimbo wake wa hivi majuzi uitwao “HISS”.

Kulingana na TMZ, hakuna kilichotokea kwenye kaburi hilo, lakini maafisa wako katika hali ya tahadhari.

Mzozo huo ulianza Ijumaa baada ya Nicki kufanya kile ambacho wengi wamekiita mzaha usiofaa kuhusu mamake Megan kwenye jukwaa la utiririshaji la Stationhead.

Maneno yake haswa yalikuwa, "Afadhali uende kumpa ujauzito mama yako na kuomba msamaha. Hiyo ni chukizo," ambayo baadhi ya mashabiki wake wanaonekana kuizingatia, TMZ imesema.

Megan, ambaye huita Houston nyumbani, amekuwa wazi kuhusu jukumu la mama yake katika maisha yake.

Katika wimbo wake wa awali ulioitwa "Cobra", Megan alielezea matatizo yake ya afya ya akili, ikiwa ni pamoja na mawazo ya zamani ya kujiua na uzoefu wake wa huzuni, ambao umemuathiri tangu mama yake na bibi yake walipofariki mwaka wa 2019, pamoja na kupigwa risasi na rapa Tory Lanez.

Nicki baadaye alieleza kuwa alimtaja tu mama yake Megan kwa sababu Megan alizungumza na mumewe Kenneth Petty aliporejelea katika wimbo wake "Megan's Law", ambayo wengi wamedhani ilikuwa kuhusu matatizo ya kisheria ya Petty, TMZ inasema.