Babymama wa Shakib amdhalilisha na kumwanika kuwa anategemea Zari kwa kila kitu

Mrembo huyo alimtia kwenye kikaango cha aibu Shakib Cham na kumtaka kutafuta kazi ya maana ya kufanya badala ya kuwekwa na mwanamke mwenye pesa zake – Zari.

Muhtasari

• “Unamuona huyu Mtu? Ndiye mwanamume asiye na utu kabisa ambaye nimewahi kutana naye duniani." alisema.

amemsherehekea mke wake Zari Hassan.
Shakib amemsherehekea mke wake Zari Hassan.
Image: INSTAGRAM// SHAKIB CHAM

Mama mtoto wa Shakib Cham, Tusiime Jalia Cremy kwa mara nyingine tena amejitokeza kwenye mitandao ya kijamii na kumtaja kuwa baba wa mtoto wao anayewajibika.

Mrembo huyo alimtia kwenye kikaango cha aibu Shakib Cham na kumtaka kutafuta kazi ya maana ya kufanya badala ya kuwekwa na mwanamke mwenye pesa zake – Zari.

“Unamuona huyu Mtu? Ndiye mwanamume asiye na utu kabisa ambaye nimewahi kutana naye duniani. Nimekuwa kimya muda wote huu kwa sababu sikuwahi kutaka kuongea ili watu waseme natafuta umaarufu na kujivunia huko...Lakini jambo moja Sitavumilia ni mtu anayemjia mwanangu kwa matusi kwa sababu ya baba yake aliyechagua kutowajibika,” alisema.

Kulingana naye, alimwendea mke wa Shakib, Zari Hassan, mara nyingi kwa sababu ya jambo hilo. Alisema wakati wa uhusiano wao, yeye ndiye alikuwa akimfadhili Shakib, na anadai kuwa Zari pia anafanya hivyo, jambo ambalo sosholaiti huyo anadaiwa alikiri katika mazungumzo yao.

Alimtaka Shakib atoke nje akafanye kazi ya kujikimu badala ya kumtegemea Zari. Jalia alisema kuwa atatoa ushahidi wa mazungumzo yake na Zari.

"Nilizungumza na Zari mara nyingi sana kuhusu suala hili na nina rekodi zote na nitatoa risiti kwa sababu Mwaka huu wa 2024 hakuna mtu ambaye ataninyamazisha kwa sababu niliweka dau ungekuwa wewe !! Plus acha kusema ni wivu maana nipo kwenye mahusiano mapya kabisa ya mtanashati 😂 nilichoka kumtunza yule ki bogus boy coz nze nkyeyiya alikula ndi kito 😂 Kushika mimba Kwa miaka 22 ugenini alikula ngateko olabilila omusaja kuzimu noooo 😂 Ninachoweza kusema ni kwamba Shakib Cham nenda kafanye kazi !! Maana hata Zari yakoowa okumusaba Buli kimu okuva ku Yaka wa 10k Yaka😂😂 aliniambia ubinafsi wake kwenye rekodi nilizo nazo. Wacha wakatae natoa risiti sagala kunkooya,” alisema.

Shakib na Zari the Bosslady hawajasema lolote kuhusu madai hayo. Hajawahi kuonekana na mtoto wake hapo awali.