Kodi yangu ya nyumba kwa mwezi ni shilingi 350K - Amber Ray

Juzi-kati Amber Ray aliwaonyesha mashabiki wake jumba lake la kifahari likiwa limekamilishwa na kambarau ambapo alishuka na kuelekea kwenye sebule yao ya kifahari.

Muhtasari

• Mama wa watoto wawili alionyesha nyumba yake mpya, kamili na lifti.

•Katika video hiyo, alishuka kutoka kwenye lifti, ambayo ilifungua moja kwa moja kwenye sebule yake, akitembea hadi kwenye ukumbi akiwa na glasi ya mvinyo mkononi.

Amber Ray na Kennedy Rapudo
Wapenzi// Amber Ray na Kennedy Rapudo
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Amber Ray amefichua kwamba kwa kila mwezi, yeye na mpenzi wake Kennedy Rapudo hulipa kodi ya nyumba Zaidi ya shilingi za Kenya laki tatu.

Ray alikuwa anamjibu kwa kumkosoa mwanablogu mmoja ambaye alikuwa makini kugundua kwamba Amber Ray na mpenzi wake wamebadilisha mazingira ya nyumba walimokuwa wakiishi hapo awali.

Mwanablogu huyo alipakia video ya Amber Ray akiwa anashuka katika ngazi za nyumba hiyo na kufichua kwa jicho la udadisi kwamba huenda Amber Ray na Kennedy Rapudo walihama kamazi yao ambapo walikuwa wakilipa kodi ya laki mbini na nusu kwa mwezi.

Alisema kwamba wawili hao walihamia nyumba nyingine ya kifahari yenye vyumba vitano ambayo kodi yake ni shilingi laki tatu.

“Inaonekana ni kama Amber Ray na babydaddy wake walihama katika makazi yao ya kifahari yenye kodi ya kila mwezi 250k na kuhamia nyumba nyingine ya kifahari yenye vyumba 5 ambayo kodi ni 300k,” Mwanablogu huyo alidadisi.

Hata hivyo, Amber Ray alifika kwenye chapisho hilo na kumkosoa mwanablogu huyo kwamba si 300k bali ni 350k, akimtanga kuzingatia hiyo elfu 50 ya juu.

“Weeeeh si 300k ni 350k tafadhali, mbona mnatoa hiyo 50k?” Ray aliuliza.

Juzi kati, sosholaiti huyo mwenye maisha laini na mfanyabiashara mume wake, Rapudo  waliwafurahisha mashabiki wao kwa kushiriki video ya makazi yake mapya ya kifahari.

Mama wa watoto wawili alionyesha nyumba yake mpya, kamili na lifti. Katika video hiyo, alishuka kutoka kwenye lifti, ambayo ilifungua moja kwa moja kwenye sebule yake, akitembea hadi kwenye ukumbi akiwa na glasi ya mvinyo mkononi.