Mwigizaji maarufu Jackie Matubia anashiriki kwenye mahojiano kwamba ingawa alikuwa na ndoa mbili zilizofeli, yeye ni mama mwenye fahari kwa watoto wake wawili.
Aliendelea kusema kuwa jamii ya leo inaelekea kuwadharau akina mama wasio na waume lakini hatakubali jambo hilo kamwangushe.
“Sitaacha jamii inidharau, Hapana! Ninajivunia mimi ni nani na ninataka kuwafundisha wasichana wangu kuwa ni sawa. Ikiwa haifanyi kazi, sio mwisho," Jackie alisema.
Jackie alitaja kuwa ndoa zake zilizofeli hazikumkatisha tamaa kwenye ndoa bali zilileta mwanga mpya kwani sasa anajua kuwa hakuna mwanamke anayepaswa kughairi.
Hii ni siku baada ya aliyekuwa mumewe Blessing Lung’Aho kuchapisha mpenzi wake mpya kwenye mitandao ya kijamii.
Wawili hao walitengana baada ya kuwa kwenye ndoa kwa chini ya miaka miwili. Kwa pamoja walipata mtoto wa kike ambaye ana mwaka mmoja sasa.
"Kwa sasa ninalenga kulea watoto wangu na kuwajengea himaya," Mama huyo wa watoto wawili alisema.
Amewashauri wasichana na wanawake wachanga wanaolea watoto kwa kujitegemea kukumbatia wao ni nani na wasiruhusu neno ‘single mama’ liwafafanulie.
"Wacha tukumbatie sisi ni nani na tusikimbilie kwa sababu unaogopa umri unakupata." Jackie alishauri.
Jackie pia aliongeza kuwa ndoa ni kitu kizuri na bado anaamini inafanya kazi.