Stevo Simple Boy atumia wimbo kumchamba KRG the Don kwa kumuita kilema (video)

“Hebu tulia weka kiburi kando. Hit song zako zote zimekuwa collabo sasa kijana tulia na uweke kiburi kando,” Rapa Stevo alimshauri KRG katika wimbo wake.

Muhtasari

• “Fresh Barida ili-hit mpaka ng’ambo hata nikicheka nazungumziwa kwa mtandao” Stevo alizidi kuonesha ukali wake kwenye mistari.

• Hata hivyo, inapaswa kujulikana kwamba Stevo ndiye alianzisha ugomvi na KRG kwa kumtaja kama vixen wa kwenye video za Sanaa.

Stevo na KRG
Stevo na KRG
Image: Facebook

Rapa Stevo Simple Boy katika njia nyingine ya kuonesha kiwango cha kukerwa kwake na tamko la msanii wa Dancehall, KRG the Don kumuita kilema, ameingia studioni na kurekodi diss track yenye hisia kali akimchamba msanii huyo kwa tamko hilo.

Mwimbaji huyo wa Fresh Barida katika diss track hiyo, amedai kwamba KRG the Don ni mwimbaji ambaye hajui kuimba n kinachomweka mjini ni kelele na tantarira zake katika mitandao ya kijamii, huku akizitaja ngoma zake zote kama ni za kusaidiwa na wasanii wengine, yaani kolabo.

“Hebu tulia weka kiburi kando. Hit song zako zote zimekuwa collabo sasa kijana tulia na uweke kiburi kando,” Rapa Stevo alimshauri KRG katika wimbo wake.

Katika wimbo huo unaoitwa Kilema, rapa Stevo anasema anataka kumpigia makofi msanii wa dancehall ambaye anapenda kutoa sumu kwa watu bado muziki na yeye mwenyewe ni kama mafuta ya taa na maji.

“Kuna msanii nataka kumchamba huku mjini ana shamba. Nataka kumwonesha yeye si msanii ni vixen. Ana kelele nyingi na hajui kuimba” Stevo anamchafua KRG kupitia mistari yake.

Zaidi katika wimbo wa diss track, rapper huyo anadai KRG anapaswa kujishusha chini na kujifunza muziki au kujitosa kwenye kitu kingine na sio muziki kama taaluma yake au kazi yake.

Anamshauri KRG kuacha kutumia dawa za kulevya kwa sababu yeye ni rapper maarufu tofauti na yeye ambaye nyimbo zake zilivuma.

Isitoshe, anaendelea na kujigamba kwamba ingawa KRG kila mara humcheka na pia humdharau, anatambulika duniani kote na kwamba hata akithubutu kucheka mtandaoni, watu hupata cha kumzungumzia.

“Fresh Barida ili-hit mpaka ng’ambo hata nikicheka nazungumziwa kwa mtandao” Stevo alizidi kuonesha ukali wake kwenye mistari.

Wimbo huo wa diss unakuja wiki kadhaa baada ya KRG kwenda hewani na kumwita Stevo mlemavu na kuongeza kuwa hawezi kufanya kazi au kubishana naye.

Hata hivyo, inapaswa kujulikana kwamba Stevo ndiye alianzisha ugomvi na KRG kwa kumtaja kama vixen wa kwenye video za Sanaa.

Bifu lao linaweza likafuatiliwa hadi miezi 10 nyuma ambapo Stevo alisema hamjui KRG ni nani wala hajawahi lisikia jina lake, jambo lililomfanya KRG kumjibu vikali kwa kusema kwamba sura yake inakaa kama kinyago cha kutisha ndege na wanyama shambani, kwa kimombo scarecrow.