Bobi Wine: Nina miaka 12 tangu niache kutumia pombe!

Wine alikuwa anamjibu mtu aliyesema amepata ugumu wa kuacha pombe ikiwa ni siku ya 9 tu baada ya kuacha kutumia pombe kwa mshangao, Wine alimwambia kwamba yeye ana miaka 12.

Muhtasari

• Salvado alikuwa anatoa maoni kwa mashabiki wake kwamba ni vigumu kwa mtu kuacha kutumia pombe katika sehemu yoyote na bado kuwa na furaha.

Maarufu kama Bobi Wine amedai kwamba hajawahi tumia pombe kwa miaka 12
Robert Kyagulanyi// Maarufu kama Bobi Wine amedai kwamba hajawahi tumia pombe kwa miaka 12
Image: Facebook//BobiWine

Msanii wa Uganda ambaye pia ni mwanasiasa maarufu wa upinzani, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine amewashangaza mashabiki wake wengi baada ya kudai kwamba ana miaka 12 tangu aache kutumia vilevi vya aina yoyote.

Mwanasiasa huyo wa chama cha upinzani, NUP alifichua haya wakati anajibu kwenye chapisho la mchekeshaji Patrick Salvado katika mtandao wa X.

Salvado alikuwa anatoa maoni kwa mashabiki wake kwamba ni vigumu kwa mtu kuacha kutumia pombe katika sehemu yoyote na bado kuwa na furaha.

Mchekeshaji huyo alisema kwamba yeye ana siku 9 tu bila pombe lakini ameona wakati mgumu, jambo ambalo limemfanya kuwaheshimu wale watu ambao hawajawahi kutumia pombe iwe katka vilabu vya pombe au kwenye tafrija na bado wana uwezo wa kupata furaha yao.

“Watu ambao hawanywi pombe kwenye vilabu au mgahawa au kwenye karamu, lakini wana furaha .. Ninawaheshimu .. eh eh eh ... sio rahisi mimi nimedhamiria kuishi maisha yenye afya #Siku9 #BilaPombe,” Salvado aliandika

Hapo ndipo msanii na mwanasiasa Bobi Wine alimjibu akifunguka kwamba yeye ana miaka 12 bla kugusa kileo chochote.

Wine alisema kwamba ana ushauri wa ajabu jinsi anaweza mshauri mtu kuacha pombe na kupotezea kabisa fikira ya kiu cha pombe, lakini aliwataka wenye uhitaji wa ushauri huo kuzungumza naye kwa njia nzuri.

“Ni mwaka wa 12 kwangu. Niongeleshe vizuri, nina maelezo. Inaweza kufikiwa,” Wine alijibu.

Mwanasiasa huyo amekuwa akihangaishwa na utawala wa NRM ukiongozwa na rais Yoweri Museveni ambaye anajaribu mbinu zote kuzikandamiza harakati zake haswa baada ya kuonekana kwamba vija na wengi wapo nyuma yake wakipigia debe upatikanaji wa mageuzi katika uongozi wa nchi.

Hivi majuzi, Wine aliwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani kwa siku kadhaa baada ya vikosi vya usalama kukita kambi nje ya boma lake usiku na mchana kumzuia asiweze kutoka ili kushiriki katika maandamano ambayo yalikuwa yameratibiwa na upinzani.