Haji Manara afichua kilichomtokea Diamond enzi za ujana wake mpaka sasa hataki kuoa

“Akikuhadithia unaona kabisa huyu amesha athirika,” Manara aliongeza katika mahojiano na Clouds TV.

Muhtasari

• Kwa upande wake, Haji Manara amekuwa akijaribu guu lake katika ndoa, akifunga ndoa mara kwa mara na kuachika baadae.

• Hivi majuzi alifunga harusi na mrembo Zaylissa ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa msanii wa Singeli, Dulla Makabila.

Manara asema Diamond alipigwa singa ujanani
Sababu ya Diamond kutooa// Manara asema Diamond alipigwa singa ujanani
Image: Facebook

Aliyekuwa msemaji wa timu za soka za Simba SC na Yanga ambaye pia ni mwandani wa karibu wa msanii Diamond Platnumz amefichua makubwa kuhusu sababu kuu ya Diamond kutotaka kuoa mpaka sasa.

Wengi wamekuwa wakimshangaa Diamond kutotaka kutulia katika ndoa licha ya kubarikiwa na mali akiwa kijana lakini mpaka sasa karibia umri wa miaka 35, msanii huyo amesalia kuwa baba kwa watoto 4 bila ndoa.

Sasa rafiki yake Manara ameamua kutumbua kile kilijiri enzi za ujana wa msanii huyo ambacho kilisalia kama kovu la kudumu katika moyo wake na kumpa mashaka ya kuoa mpaka sasa.

“Nasib [Diamond] unajua ni muoga wa kuoa. Na Nasib unajua alipata nadhani katika uvulana wake, alipigwa dafrau moja na binti, sijui hata ni binti yupi na hata sitaki kumtaja. Ilimfanya anakuwa anawaogopa kweli wanawake, hatengenezi uaminifu wa asilimia mia kwao mpaka sasa,” Manara alifichua.

“Yaani ni ile wanawake walimpigaaa kupitiliza. Tukikaa naye ananiambia lakini siwezi kumtaja, kwa hiyo lile linamfanya kusita sana linapokuja suala zima la ndoa. Unajua ukipigwa pigo kubwa tena…” Manara aliongeza.

Alisema kwamba Diamond kuzungumzia suala hilo litamchukua hadi saa 3 nzima kuhadithia kwani ni makubwa sana yaliyomkuta kipindi hicho.

“Akikuhadithia unaona kabisa huyu amesha athirika,” Manara aliongeza katika mahojiano na Clouds TV.

Diamond amekuwa akijaribu uhusiano tangu enzi hizo alipoanza na Wema Sepetu, akaja akapata watoto wawili na Zari Hassan, baadae mtoto mmoja na Hamisa Mobetto na pia mmoja na Tanasha Donna lakini wote waliishia kuwa wapenzi tu wenye watoto pasi na kufunga harusi.

Kwa upande wake, Haji Manara amekuwa akijaribu guu lake katika ndoa, akifunga ndoa mara kwa mara na kuachika baadae.

Hivi majuzi alifunga harusi na mrembo Zaylissa ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa msanii wa Singeli, Dulla Makabila.