Utahitaji kumlipa msanii Notiflow kima cha shilingi 160k ili kuku'follow Instagram

Notiflow alisema kwamba mtu yeyote ambaye anam’follow Instagram na anataka yeye [Notiflow] kufanya follow-back basi atahitaji kulipa dola elfu moja, sawa na 160,500 pesa za Kenya.

Muhtasari

• “Na kufikia wiki ijayo bei inapanda,” Notiflow aliongeza.

• Katika ukurasa wake wa Instagram, Notiflow ana wafuasi wapatao 931k huku yeye akiwa hana mtu hata mmoja ambaye anam'follow.

Notiflow
Notiflow
Image: Instagram

Natalia Florence, maarufu kwa jina la kisanii kama Notiflow amefichua kwamba analipisha kiasi cha laki moja na elfu 60 pesa za Kenya ili kutengeneza urafiki na mtu katika mtandao wa Instagram, maarufu kama ‘follow back’.

Msanii huyo alivujisha mawasiliano na mtu mmoja katika DM yake ambaye alikuwa anataka watengeneze urafiki wa kufuatana kaitka mtandao huo wa picha.

Notiflow alisema kwamba mtu yeyote ambaye anam’follow Instagram na anataka yeye [Notiflow] kufanya follow-back basi atahitaji kulipa dola elfu moja, sawa na 160,500 pesa za Kenya.

“Ili kupata follow ya malkia Noti, ni dola elfu moja pekee,” aiandika kwenye chapisho hilo.

Baada ya tangazo hilo lake kuenezwa mitandaoni, Notiflow alirudi na kusema kwamba ifikapo wiki kesho, bei hiyo itapanda mara dufu hivyo kuwataka wanaotaka kuwa marafiki zake kwenye Instagram kuchangamkia fursa wakati bado bei ni dola elfu moja pekee.

“Na kufikia wiki ijayo bei inapanda,” Notiflow aliongeza.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Notiflow ana wafuasi wapatao 931k huku yeye akiwa hana mtu hata mmoja ambaye anam'follow.

Mpenzi huyo wa zamani wa rapa Colonel Mustafa amekuwa akizungumziwa kwenye vyombo vya habari katika kipindi cha miaka ya nyuma kutokana na uhusiano wake tata na mwanamke mwenzake, King Alami.

Wawili hao walisemekana kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na wakati Alami alidondoka kutoka ghorofani mwaka jana, Notiflow alijitokeza na kusema kwamba ni yeye wa kulaumiwa kwani Alami alidondoka kutokana na msongo wa mawazo ya huba lao kutokuwa sawa.