Mtetezi mkali wa sera za kinara wa ODM Raila Odinga, Nuru Okanga kwa mara nyingine tena yuko kwenye vichwa vya habari za udaku.
Hii ni baada ya kufichua kwa furaha kwa wafuasi wake katika mtandao wa Facebook kwamba baada ya kuhudhuria masomo ya kidato cha kwanza kwa mwezi mmoja, hatimaye ameng’amua maana halisi ya somo ya sayansi – Biolojia.
Okanga kwa furaha alieleza kwamba amefurahi kufahamu maana ya somo hilo ambalo amekuwa akilisikia midomoni mwa wenzake ambao walimtangulia kuingia kidato cha kwanza, ikiwa ni miaka kadhaa baada yake yeye kushindwa kuendelea na masomo yake kufuatilia kifo cha babake – kama alivyoeleza awali katika mahojiano na Radio Jambo.
Okanga alisema kwamba biolojia si ngumu kwani aligundua ‘bio’ ni somo kuhusu maisha na ‘olojia’ ni somo lenyewe.
“UFAFANUZI RAHISI WA BIOLOJIA. Bio unamaanisha maisha na -olojia inamaanisha "kusoma" kwa hivyo biolojia inamaanisha kusoma maisha. Biolojia ni somo la viumbe vyote hai (na viumbe vilivyokufa, kama vile visukuku). Biolojia inaangalia jinsi viumbe hivi vinavyounda, kuendeleza na kuingiliana na kila mmoja na mazingira yao,” Okanga alieleza kwa furaha.
Aliendelea kumjibu mfuasi aliyehoji kwa nini anashiriki ufafanuzi huo, akisema alikuwa shuleni kujifunza, si kuwakodolea macho walimu.
"Nilienda kusoma sio kuangalia walimu tu (nilienda shule kusoma, sio kuwakodolea macho walimu)," Okanga alijibu.
Okanga alikuwa katika vichwa vya habari mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuwa miongoni mwa watahiniwa wakongwe Zaidi kuketi kufanya mitihani ya darasa la nane KCPE.
Hata hivyo, baada ya matokeo kutoka, Okanga alikuwa msiri kufichua alama alizozipata na hata kwenye mahojiano na Radio Jambo, kijana huyo mwenye azma ya kuwania kama MCA katika uchaguzi mkuu wa 2027.