Diamond aongoza wasanii kumpa hongera Rayvanny kwa kuangukia dili nono Marekani

Rayvanny alidokeza kwamba ameoata dili ya mamilioni ya dola nchini Marekani ambalo ataliweka wazi hivi karibuni.

Muhtasari

• "Multimillion dollar deal, ilikua ni ndoto yangu ya muda mrefu sana , God is good. Global way, global deal in us," Rayvanny aliandika.

Rayvanny
Rayvanny
Image: Instagram

Msanii gwiji wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amewaongoza wasanii wa Kitanzania kutuma risala za pongezi na hongera kwa aliyekuwa msanii chini ya lebo yake, Rayvanny kwa kupata dili nono la mamilioni ya dola nchini Marekani.

Rayvanny alithibitisha kuangukia dili hilo nono nchini Marekani kupitia ukurasa wake wa Instagram, japo hakuweka wazi ni dili lipi hilo.

Msanii huyo aliyeondoka WCB Wasafi mwaka 2022 na kuanzisha lebo yake binafsi ya Next Level Music alisema kwamba ni ndoto iliyotimia kupata dili hilo litakalomwezesha kutia kibindoni mamilioni ya dola za Kimarekani.

"Multimillion dollar deal, ilikua ni ndoto yangu ya muda mrefu sana , God is good. Global way, global deal in us," Rayvanny aliandika.

Licha ya kutofichua kwa mashabiki wake ni dili gani hilo, ‘baba yake’ kimuziki, Diamond Platnumz aliwaongoza wenzake kumpa hongera lakini pia kumtakia kila la kheri katika safari hiyo mpya.

“Super proud of you Vanny Bway, I cannot wait for your new big achievement to be revealed!” Alianidika Diamond.

“Big movement bro Rayvanny,” produsa S2kizzi alimhongera.

“All the best V Vanny boy,” Billnass aliandika.

“Big moves big bag, twende kazi kaka,” Juma Jux aliandika.

Kila mtu sasa anasubiria Rayvanny kuweka wazi ni dili lipi hilo aliloliangukia nchini Marekani.