Diamond kwangu hatoki hata mmpe 'Sim 2' - Zuchu atuma taarifa kwa wanaotaka waachane (video)

Zuchu alitoa taarifa kwa mahasidi wa penzi lao upande wa pili akiwaambia kwamba kama walikuwa wanakesha wakisubiri Diamond kutoka ubavuni mwake basi wataharibu mishumaa tu hadi kukuche.

Muhtasari

• Mwishoni mwa juma, Zuchu alikwenda kwenye Instagram na kuachia ujumbe mrefu akisema kwamba amechoka kutendwa katika mapenzi.

Mama Dangote akanusha Diamond kutoka kimapenzi na Zuchu.
Mama Dangote akanusha Diamond kutoka kimapenzi na Zuchu.
Image: Screengrab//YouTube

Msanii wa kike kutoka lebo ya WCB Wasafi, Zuchu ametengua kauli yake ya siku mbili zilizopita kwamba wameshaachana na Diamond Platnumz na kuwa yuko single.

Akiwa katika shoo ya full moon party kisiwani Zanzibar pamoja na Diamond, Zuchu alisema kwamba yeye na Diamond ni kama mtoto mchanga na usingizi, kwani hawawezi kuachana leo wala kesho.

Picha na video ambazo zimesambazwa kutoka kwa tukio lao huko Zanzibar wikendi iliyopita zinawanyesha wawili hao wakiwa katika mikao ya mahaba mazito. Kinyume na kauli zao siku mbili zilizopita kwamba wameshatengana.

Zuchu wakati wa kutumbuiza kwake, aliamua kutoa taarifa kwa mahasidi wa penzi lao upande wa pili akiwaambia kwamba kama walikuwa wanakesha wakisubiri Diamond kutoka ubavuni mwake basi wataharibu mishumaa tu hadi kukuche.

“Ila wacha tutume taarifa kwa upande wa pili si ndio? Wanaohisi watamchukua [Diamond], nawaona mnamaliza Miungu, mnamaliza mikao na utundu, huyu kwangu hapa hatoki hata mmpe mkun**,” Zuchu aliimba.

Mwishoni mwa juma, Zuchu alikwenda kwenye Instagram na kuachia ujumbe mrefu akisema kwamba amechoka kutendwa katika mapenzi na ameshafikia hatua ya kuwa bila mpenzi.

“HABARI FAMILIA .ILIBIDI KUPOST HII ILI KUFUTA DHAMIRI YANGU. KUANZIA LEO HII MIMI NA NASIBU (DIAMOND) HATUKO PAMOJA,” Zuchu alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Aliongeza, “NAJUA HILI LIMEKUWA JAMBO LETU LAKINI AS HARD AS IT IS KUMUACHA MTU UNAEMPENDA HII NAOMBA MUNGU IWE YA MWISHO NA NIANZE MAISHA MAPYA. MAPENZI NI HESHIMA KWA BAHATI MBAYA SANA HIKO KIMEKOSEKANA KWETU.”

Hii ni baada ya kuibuka kwa video ya Diamond na babymama wake Zari wakiwa wameshikana mikono wakitembea kwa mwendo wa taratibu, Diamond akimtaja Zari kama ‘dadangu’.