Zari akiri kuwepo kwa matatizo katika ndoa yake na Shakib, kuhusu picha yake na Diamond...

Alifichua kwamba video akiwa ameshikana na Diamond ilikuwa ni tangazo la kibiashara tu lakini ilitafsiriwa visivyo na Shakib, na hivyo kumuomba msamaha kwa kutomueleza kabla kuhusiana na video hiyo.

Muhtasari

• Alisema kwamba Diamond sio chanzo cha Shakib kukasirika na kufuta picha zake [Zari] kwenye ukurasa wake.

• Zari hata hivyo alisema kwamba penzi lake na Shakib bado lipo sana na hakuna chochote kitakacholisambaratisha.

Shakib na Zari
Shakib na Zari
Image: Instagram

Mjasiriamali maarufu kutoka Uganda Zari Hassan amefunguka kwa mara ya kwanza kinachoendelea katika ndoa yake na Shakib Lutaaya Cham ambapo wawili hao mara kwa mara wanasemekana kufuta picha za kila mmoja kutoka kwenye kurasa zao kwenye Instagram.

Zari akizungumzia suala hilo, pindi baada ya Shakib kufuta picha za Zari ikikisiwa kuwa chanzo ni picha ya Zari akiwa ameshikana mikono na babydaddy wake Diamond Platnumz, Zari alisema kwamba wamekuwa na matatizo kuanzia Novemba mwaka jana.

Alisema kwamba Diamond sio chanzo cha Shakib kukasirika na kufuta picha zake [Zari] kwenye ukurasa wake.

Kuhusu uhusiano wa Zuchu na Diamond kuvunjika na kurudiana kila mara, Zari alisema kwamba yeye na Shakib wameshalizoea hilo na wala halina chochote kuhusiana na penzi lao.

Mimi na Shakib tumekuwa na matatizo yetu, nilianza kufuta picha zake kwenye Instagram yangu toka mwezi November, December tulikuwa na matatizo Big Big issues, so haiwezi kutokea sasa hivi kuwa Baba T na Zari ndio Shakib anajiweka kwenye hiyo situation au Zuchu anaenda. Zuchu kila wiki anaenda na kurudi,” alisema.

Zari hata hivyo alisema kwamba penzi lake na Shakib bado lipo sana na hakuna chochote kitakacholisambaratisha.

Mjasiriamali huyo mwenye makazi yake Afrika Kusini alifichua kwamba video yake akiwa ameshikana na Diamond ilikuwa ni tangazo la kibiashara tu lakini ilitafsiriwa visivyo na Shakib, na hivyo kumuomba msamaha kwa kutomueleza kabla kuhusiana na video hiyo.

"Shakib hajaondoka kwa sababu ya video yangu na Diamond, alikuwa ni lazima asafiri ile siku, simlaumu kujisikia anavyojisikia kwa sababu sikumwambia kuhusu ile video kama ni ya promo so amejisikia kama nimemvunjia heshima, kutoka moyoni namuomba msamaha," Zari alisema kutoka moyoni.

Juzi-kati Diamond alionekana kwenye video wakiwa wameshikana mikono kama wapenzi na mama huyo wa wanawe wawili na kumtaja kuwa ni ‘dada yangu’.

Baadae, Shakib alifuta picha zote za Zari kwenye Instagram na kutoa ujumbe ulioonyesha kwamba hakuwa amefurahishwa na kitendo cha Zari kuonekana mara kwa mara na aliyekuwa mpenzi wake.