Stevo Simple Boy ataja mipango yake ya kimaisha ya Betty Kyalo endapo atamkubalia kumuoa

Msanii huyo aliyewahi toka kimapenzi na Pritty Vishy alisema kwamba katika tumbo la Betty Kyallo, anawaona wanawe 3 – wavulana wawili na msichana mmoja.

Muhtasari

• Stevo anaendelea kumfukuzia Betty Kyallo licha ya kwamba amekuwa akiwaaminisha mashabiki wake kwamba mkewe Grace Atieno yuko na ni mjamzito.

Stevo amtongoza Betty Kyallo
Stevo amtongoza Betty Kyallo
Image: Instagram

Msanii Stevo Simple Boy amefunguka kwa mapana na marefu kuhusu mipango yake ya kimaisha na mwanahabari Betty Kyalo endapo mama huyo wa mtoto mmoja atakubali ombi lake la kuoana.

Kupitia Instagram, raoa huyo wa ‘Freshi Barida’ amekuwa akisindika maneno ya kumchombeza Betty Kyalo kumkubalia kumuoa, jambo ambalo hata hivyo Kyallo amelipa sikio la kiziwi.

Safari hii Stevo amerejea tena akitoa mipango yake kwamba endapo atapata ndio ya Betty Kyallo kuingia katika ndoa naye, basi atafanya uamuzi wa kutulia mara moja wala hatorudi sokoni tena.

Msanii huyo aliyewahi toka kimapenzi na Pritty Vishy alisema kwamba katika tumbo la Betty Kyallo, anawaona wanawe 3 – wavulana wawili na msichana mmoja – na kumtaka Kyallo kukubali kabla muda haukwenda.

“Mimi nikimpata Betty Kyalo natulia tu katika ndoa. Halafu anizalie watoto watatu, wavulana wawili na msichana mmoja. Mungu bariki maana hii yote uliumba wewe mwenyewe. Naomba sasa unibariki nayo,” Stevo aliandika huku akiichapisha picha ya Betty Kyallo.

Stevo anaendelea kumfukuzia Betty Kyallo licha ya kwamba amekuwa akiwaaminisha mashabiki wake kwamba mkewe Grace Atieno yuko na ni mjamzito.

Hili limefanya baadhi kuhisi kwamba msanii huyo kutoka Kibera anafukuzia kiki kwa kutumia jina la Betty Kyallo.

Kwa upande wake, Kyallo – mama wa binti mmoja – amekuwa na nuksi katika suala zima la ndoa, huku kila uhusiano anaoujaribu ukiyumba na kuishia kuwa kero.

Tangu ndoa yake ya kifahari na mwanahabari mwenza Dennis Okari, ndoa ambayo ilivunjika miaka michache baadae, mjasiriamali huyo wa FlairbyBetty hajakuwa na kismati katika ndoa.

Lakini je, atalikubali ombi la Stevo ama atazidi kulifumbia macho?