Mwili wa sixpack wa Alikiba wampagawisha Maua Sama na kumuacha akitamani penzi lake

Mkali huyo wa ‘iokote’ alisema kwamba mwaka jana aliharibikiwa na mimba na ni jambo ambalo mpaka leo hii hapendi kabisa kulizungumzia kwa sababu linamuumiza sana na kumkumbusha machungu.

Muhtasari

• Alimtaja Alikiba kama msanii ambaye ana moyo mweupe sana katika suala zima la kutoa sapoti kwa msanii yeyote.

Alikiba, Maua Sama
Alikiba, Maua Sama
Image: Facebook

Maua Sama, msanii wa kike wa Bongo Fleva ameonyesha mahaba yake wazi wazi kwa bosi wa lebo ya Kings Music, Alikiba.

Sama akizungumza na wanablogu, alitetea hatua yake ya kutumia picha ya Alikiba kwenye utambulisho wa ukurasa wake wa Instagram, na kusema kwamba kando na kufukuzia kiki kwa ajili ya ngoma yake mpya, pia anampenda Alikiba kutoka ndani ya moyo wake.

Alimtaja Alikiba kama msanii ambaye ana moyo mweupe sana katika suala zima la kutoa sapoti kwa msanii yeyote.

Kando na hilo, Sama pia alisema kwamba mwili wa sixpack wa Alikiba unamnyima usingizi kila mara anapoona picha zake, jambo lililomchochea kuitumia moja ya picha zake kama DP ya Instagram.

“Nampenda Alikiba, kusema kweli na pia kwenye suala zima la... si unajua umetoa nyimbo lazima utengeneze upepo. Hamna shida katka hilo. Lakini pia nampenda Alikiba kutoa mfunguni mwa moyo wangu kwa sababu yeye ni msanii ambaye ako vizuri na pia wakati inakuja kwa kukupa sapotim anafanya hivyo 100%,” Sama alisema.

“Lakini pia ana mwili mzuri sana, lakini yeye kwangu ni kama kakangu. Na mimi kama dadake ninakubali sana jinsi mwili wake unavyomtoa. Sijawahi mwambia hivyo kwa sababu namchukulia kama kaka yangu,” aliongeza.

 Mrembo huyo ambaye amekuja na wimbo mpya baada ya mwaka wa 2023 wenye changamoto nyingi upande wake alisema kwamba aliathirika pakubwa kisaikolojia baada ya kuharibikiwa na mimba.

Mkali huyo wa ‘iokote’ alisema kwamba mwaka jana aliharibikiwa na mimba na ni jambo ambalo mpaka leo hii hapendi kabisa kulizungumzia kwa sababu linamuumiza sana na kumkumbusha machungu.

“Kwenye muziki mwaka jana haukuwa mzuri kwangu, niliharibikiwa na mimba mwaka jana, nilipata changamoto kidogo kwenye uzazi lakini niko sawa. Sio stori ambayo napenda kuizungumzia sana, ni moja ya jambo ambalo lilinipa changamoto na nikajaribu kuchukua likizo kidogo, lakini nimerudi sasa, na natumai itaniwia vizuri,” alisema.