logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harmonize adokeza Hanstone wa 'iokote' kuchukua nafasi ya Anjella Konde Gang

Hanstone alipanda kwenye chati za umaarufu baada ya kolabo ya 'iokote' na Maua Sama.

image
na Davis Ojiambo

Burudani29 February 2024 - 11:54

Muhtasari


  • • Hanstone alipata umaarufu Zaidi mwaka 2019 kufuatia ufanisi mkubwa wa kolabo yake ya ‘iokote’ na Maua Sama
Harmonize amvuta Hanstone Konde Gang

Wiki moja baada ya kutangaza ujio wa wasanii wengine wawili chini ya lebo ya Konde Gang, Harmonize anazidi kuwapa mashabiki wake viashiria vyote kuhusu utambulisho wa vipaji hivyo vipya vitakavyojiunga naye muda si mrefu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize alipakia msururu wa mazungumzo kwenye DM yake na msanii Hanstone.

Hanstone alipata umaarufu Zaidi mwaka 2019 kufuatia ufanisi mkubwa wa kolabo yake ya ‘iokote’ na Maua Sama.

Tangu kipindi hicho, amekua akiachia ngoma lakini ndio hivyo tena hajakuwa akisikika sana kama ambavyo alisikika kipindi ‘iokote’ ipo katka anga za juu kwenye malimwengu ya muziki.

Harmonize baada ya kuonyesha mazungumzo yao, aliwauliza mashabiki wake ikiwa wataridhia yeye kumchukua kama mrithi wa nafasi iliyoachwa na Anjella aliyetimka mwaka juzi.

Alimtaja Hanstone kama kipaji cha kweli na kuuliza kama itakuwa sawa kwake yeye kuacha kipaji hicho kupotea hivi hivi.

“Can we let really talent die Au tumuunganishe Na Chama Linalo Mtegemea MUNGU, Konde Gang?” Harmonize aliuliza.

Hii inakuja siku mbili tu baada ya Harmonize kuweka wazi kwamba kwa sasa Konde Gang sio lebo bali ni jeshi la watu wawili tu – yeye na Ibraah na kutangaza kwamba ataongeza wengine wawili ili wawe jeshi la watu wanne.

Itakumbukwa Hanstone aliwahi kuhusishwa na kwenda WCB Wasafi kuziba pengo lililoachwa na Rayvanny lakini uvumi huo ukaja kuzima kabla ya Dvoice kutambulishwa kama mrithi halali wa nafasi hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved