'Nilimsikitikia sana Zuchu' Shakib avunja kimya kuhusu video ya Diamond na Zari (video)

"Kuna video fulani ambazo huenda zaidi ya uzazi wa kushirikiana," Shakib alisema

Muhtasari

• "Sijui jinsi alihisi lakini nilihisi vibaya kwa ajili yake," alisema.

Zari, Diamond na wapenzi wao
Zari, Diamond na wapenzi wao
Image: Instagram

Kwa mara ya kwanza, Shakib Lutaaya Cham amevunja kimya kuhusu video ya Diamond na Zari wakitembea kwa mwendo wa kimahaba huku wameshikana mikono.

Katika kionjo cha mazungumzo yao ya kina ambayo walifanya na Mange Kimambi, Shakib alisema kwamba video ile inamfanya kumsikitikia Zaidi Zuchu kuliko kujisikitikia yeye mwenyewe.

Kijana huyo anayesemekana kufungasha virago vyake na kuondoka kwa Zari baada ya kuona video hiyp Zari akiwa anatembea na baba wa wanawe wawili, alisema kwamba kwa kweli inavunja hisia za Zuchu Zaidi kuliko mtu yeyote yule.

"Sijui jinsi alihisi lakini nilihisi vibaya kwa ajili yake," alisema.

Mwenyewe alidhihirisha hisia zake kutokana na video hiyo inayoonyesha watu wawili wakiwa katika mapenzi na kusema kwamba ilimuuma kwani inaashiria kwamba kuna kitu kinachoendelea kati yao kando na kusaidiana kuwalea watoto.

Ingawa kwa muda wote amekuwa akipenda kuhusu Zari kukutana na kushiriki nyakati na baba yake mtoto Diamond na watoto wao, Shakib alisema wakati huu walienda mbali sana.

"Kuna video fulani ambazo huenda zaidi ya uzazi wa kushirikiana," Shakib alisema kwenye kionjo cha mahojiano aliyoshiriki Kimambi.