Sijaanza kumpenda Betty Kyallo leo, nilimpenda tangu 2019 - Stevo Simple Boy afuchua

“Betty ako na sura nzuri, ni mkarimu, mwenye roho safi na ni mtu ambaye anapenda kucheka, hicho ndicho kilinivutia kwake,” aliongeza.

Muhtasari

• Stevo alikumbuka kwamba mara ya kwanza kukutana na Betty Kyallo kipindi hicho akifanya kazi kwenye runinga ya K24.

Kyallo na Stevo
Kyallo na Stevo
Image: Facebook,

Msanii rapa Stevo Simple Boy hatimaye amevunja kimya chake kuhusu penzi lake kwa mwanahabari Bety Kyallo.

Katika mahojiano na Trudy Kitui, Stevo Simple Boy alifichua kwamba mapenzi yake kwa mama huyo wa binti mmoja hayajaanza leo bali ni dukuduku ambalo limekuwa katika moyo wake kwa Zaidi ya miaka 5 sasa.

Stevo alikumbuka kwamba mara ya kwanza kukutana na Betty Kyallo kipindi hicho akifanya kazi kwenye runinga ya K24, alijikuta amempenda na tangu wakati huo, hakuwa amepata nafasi nzuri ya kulitoa dukuduku la moyo wake.

Msanii huyo alikumbuka kwamba kilichowakutanisha na kibao chake cha kwanza, Mihadarati, ambapo Kyallo alimhoji na tangu hapo, amekuwa akimuona kama mrithi wa Pritty Vishy katika moyo wake.

“Betty nilianza kumpenda wakati Fulani 2019 nilipotoa ngoma yangu ya Mihadarati. Wakati huo alikuwa K24 alinitafuta akanihoji, hiyo stori yangu aliniambia watu waliipenda Zaidi. Hapo ndipo nilimpenda Zaidi,” alisema.

Vile vile, msanii huyo wa ‘Freshi Barida’ alisema kwamba alitumia fursa murwa ya Betty Kyallo kutengana na aliyekuwa mpenzi wake, na kuapa kwamba angepitia njia yoyote kumwahi.

“Wakati alisema kwamba mwanamume amemdanganya, sasa amebaki single, nikauliza wanaume, msichana mrembo kama huyu mbona mnamvunja moyo na mimi niko hapa. Sasa hapo tukazungumza na meneja wangu tukasema wacha tutume ombi kwa Betty, na hivyo ndivyo kumeenda,” aliongeza.

Akizungumzia kuchukua muda mrefu kumdhihirishia Betty Kyallo yaliyomo moyoni mwake, Stevo alijitetea kwamba hapo awali alikuwa anajua kwamba mrembo huyo ako kwenye uhusiano kwa hiyo hakutaka kuwa sababu ya mwanamume mwingine kulia.

“Hapo awali nilijua kwamba ako na mtu, sikujua kwamba ako single, nikianza kumpost mitandaoni, sikuwahi nimemtafuta kupitia DM, nilisema tu wacha nijaribu na ikajipa.”

“Betty ako na sura nzuri, ni mkarimu, mwenye roho safi na ni mtu ambaye anapenda kucheka, hicho ndicho kilinivutia kwake,” aliongeza.