Rayvanny afichua sababu ya kujiwa na wazo la kuongeza walinzi wake mshahara

Hii ni baada ya kupigwa na butwaa na kiasi kikubwa cha hela alichoombwa na walinzi wa Ufaransa alipohudhuria wiki ya maonyesho ya fasheni jijini Paris wiki jana.

Muhtasari

• Wiki jana akiwa jijini Paris, Rayvanny alionekana akijumuika na beki wa PSG na timu ya taifa ya Morocco, Achraf Hakimi.

Rayvanny
Rayvanny
Image: Facebook

Msanii ambaye pia ni bosi wa lebo ya Next Level Music, Rayvanny ametangaza mpango wa kuwaongeza wlainzi wake mshahara.

Hii ni baada ya kupigwa na butwaa na kiasi kikubwa cha hela alichoombwa na walinzi wa Ufaransa alipohudhuria wiki ya maonyesho ya fasheni jijini Paris wiki jana.

Rayvanny alisema kwamba alikuwa anataka mtu wa kumpa ulinzi binafsi akiwa jijini Paris lakini alipoambiwa kiasi cha hela ambacho angestahili kutoa kwa mlinzi, alibaki kinywa wazi na kugundua kwamba nyumbani [Tanzania] ndio walinzi binafsi wanabezwa kwa kulipwa mishahara duni.

Msanii huyo aliahidi kufanya marekebisho kwa mishahara ya walinzi wake binafsi.

“Kwa hela niliyoombwa na mlinzi binafsi hapa Paris, nadhani kuna haja ya kuongeza malipo kwa mlinzi wangu Tanzania,” Rayvanny alifichua kupitia ukurasa wa Instagram.

Wiki jana akiwa jijini Paris, Rayvanny alionekana akijumuika na beki wa PSG na timu ya taifa ya Morocco, Achraf Hakimi.

Hakimi anatambulika sana na wengi haswa kutokana na stori zisizothibitshwa ambazo zilienezwa pakubwa mwaka jana kuhusu talaka yake na mkewe.

Kwa mujibu wa uvumi huo, Hakimi alisemekana kuanfdikisha mali yake yote kwa jina la mamake na mkewe alipoelekea mahakamani kutaka talaka pamoja na mgao wa mali, alipigwa na butwaa kutaarifiwa kwamba mumewe hakuna na mali yoyote chini ya jina lake.