Najuta kujitunza mwishowe na nikaishia kuwa single mother - Justina Syokau

"Najuta kwamba nilipata mtoto wakati nilikuwa nimeokoka sana na niko hapa nje leo kama single mother wakati wengine ambao walikuwa wanahanya wakiwa wasichana sasa hivi wako katika ndoa."

Muhtasari

• "Kwa sababu tuliambiwa maandazi yameumwa hayawezi kupata mteja sokoni,” Justina alisema.

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau
Image: HISANI
JUSTINA SYOKAU
JUSTINA SYOKAU
Image: Facebook

Msanii wa injili mwenye utata kutoka Ukambani, Justina Syokau ni mama mwenye majuto mengi kuhusu maisha ya kihafidhina aliyokuwa akiyaishi enzi za usichana wake.

 Akizungumza kwenye Oga Obinna Live Show, Syokau alisema kwamba kama kuna kitu ambacho anakijutia sasa hivi ni kutunza usichana wake lakini akaishia kupatana na mwanamume ambaye alimzalisha ya kumuacha.

Syokau alisema kwamba alikuwa amejitunza mno kipindi akiwa shule kwani alikuwa ameokoka lakini marafiki zake ambao walikuwa wanatoka na wanaume tofauti tofauti sasa hivi wametulia kwenye ndoa ilhali yeye aliyejitunza vizuri ameishia kuwa single mother tu.

“Nafikiri wokovu ulichangia Zaidi kutokujua maisha, nilikuwa mwenyekiti wa muungano wa wanafunzi wakristo shuleni, nikianza kufanya kazi nilikuwa nimeokoka. Nilikuwa nimeuweka [ubikira] kwa ajili ya mume wangu nikidhani hii ndio kila kitu, kwa sababu tuliambiwa maandazi yameumwa hayawezi kupata mteja sokoni,” Justina alisema.

“Nafikiri ni heri ningetafuta uzoefu na kuelewa. Najuta sikujua maisha, najuta kwamba nilijitunza sana na nikaja kupata kuvunjwa moyo. Najuta kwamba nilipata mtoto wakati nilikuwa nimeokoka sana na niko hapa nje leo kama single mother wakati wengine ambao walikuwa wanahanya wakiwa wasichana sasa hivi wako katika ndoa na wametulia,” Justina alielezea mafadhaiko yake.

Tangu alipoachana na mumewe, Syokau hajawahi kupata mwanamume makini wa kuchumbiana na kuolewa. Katika mahojiano mengi, alidai kwamba wakati angepata moja yenye sifa anazohitaji kutoka kwa mwanamume, ndipo atakapoolewa.