Michael Olunga auziwa kilo moja ya avocado shilingi 623 nchini Qatar

Mchezaji huyo nguli aliwapongeza Wakulima wa Kenya akisema kwamba mazao yao ya parachichi yalikuwa yakitawala masoko ya vyakula katika taifa hilo la Kiarabu.

Michael Olunga
Michael Olunga
Image: Facebook

Mchezaji wa Al Duhail ya Qatar na ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Harambee Stars, Michael Olunga alipigwa na butwaa baada ya kuuziwa kilo moja ya avocado nchini Qatar kwa shilingi 623 pesa za Kenya.

Olunga ambaye anapenda kuwaeleza mashabiki na wafuasi wake kupitia mitandao ya kijamii jinsi anavyoishi maisha katika taifa hilo la kiarabu, alipakia picha akiwa kwenye duka moja kuu ambalo linauza vyakula.

Akiwa mbele ya kapu la parachichi, Ounga alionesha bei, akisema kwamba alitakiwa kulipa shilingi za Kenya 623 kwa ajili ya kilo moja tu ya zao hilo ambalo nchini Kenya linapatikana kwa bei nafuu.

Baada ya kununua, aliwauliza mashabiki wake haswa kutoka humu nchini akilenga kujua ni shilingi ngapi ambazo wananunua parachichi kilo moja.

“Kwenye pilka pilka ya kutafuta Avocado ya supper .  1kg =16.50Qr = 623ksh. Huko kwenyu imefika ngapi?” Olunga aliuliza.

Hata ivyo, alipokea majibu ya kushangaza, baadhi wakisema kwamba parachichi kwa kilo haifai kuzidi shilingi 150.

Mchezaji huyo nguli aliwapongeza Wakulima wa Kenya akisema kwamba mazao yao ya parachichi yalikuwa yakitawala masoko ya vyakula katika taifa hilo la Kiarabu.

Itakumbukwa mwaka mmoja uliopita, Olunga pia alionyesha kushangazwa baada ya kutakiwa kulipa shilingi 600 pesa za kenya kwa ajili ya mboga aina ya Sukuma wiki.

"Kale ya Kenya (sukuma wiki) 18.25 kwa fungo (takriban Ksh 600). Wueeeh!!!Ni ukweli Inakata pande zote mbili," Oling aliandika.

Alienda kwenye sehemu ya maoni ya chapisho hilo na kusema kuwa anafuraha kwa wakulima wa Kenya kwa kuwa mauzo yao ya nje yalikuwa yakifanya vyema katika soko la kimataifa. "Mama mboga anavuna sana. Furaha kwa wakulima wetu wa Kenya. Sukuma Wiki ya Kenya inahitajika sana . Imeisha. Hii hapa nilinunua pakiti 5 kwa 91 ( KSh 2700)."

Mchezaji huyo atakuwa anaiongoza timu ya taifa, Harambee Stars katika michuano ya kirafiki wiki hii.