Shorn Arwa aandika kitabu cha kutoa mafunzo kwa warembo jinsi ya kuwa 'wig influencer'

“Kila siku nawaambia nunua kitabu changu ili kuwa influencer wa wigi hamtaki, angalia baadhi ya vifurushi vya mawigi ambavyo nimepokea, nunua kitabu changu uwe influencer wa wigi," alisema.

Muhtasari

• Arwa kupitia akaunti yake ya Instagram, aliandika kwamba kwa sasa yuko hadi mawigi 14 lakini akaweka wazi kwamba hakuna wigi hata moja analolitoa bure kwa mtu yeyote.

Shornarwa
Shornarwa
Image: Instagram

Mhamasishaji wa mitandaoni kuhusu masuala ya mitindo ya fasheni, Shorn Arwa amefichua kwamba ana kitabu chake alichokiandika mahususi kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa watu haswa warembo jinsi ya kutumia wigi kutoa hamasisho.

Arwa kupitia akaunti yake ya Instagram, aliandika kwamba kwa sasa yuko hadi mawigi 14 lakini akaweka wazi kwamba hakuna wigi hata moja analolitoa bure kwa mtu yeyote.

Arwa aliwatembeza mashabiki wake kwenye rafu ya bidhaa zake za nywele na kusema kwamba kama kuna yeyote anayetaka kuwa influencer wa bidhaa za nywele, basi ajichukulie kitabu chake ili kubaini ni vipi anaweza akatusua katika hilo.

Aidha, mrembo huyo alisema kwamba kwa yeyote anayetaka kufaidi wigi la bila malipo kutoka kwake, japo hapeani bure – atahitaji kununua kitabu chake ili kupata wigi bila malipo.

“Habari za asubuhi jamani, kuna kitu nafaa kuweka wazi katika njia ya kiheshima kabisa, sipeani wigi lolote bila malipo. Baada ya kuyaweka, nitayauza tena. Pia ninauza kitabu jinsi ya kuwa influencer wa mawigi, kwa hiyo nunua kitabu changu ili kupata wigi la bure,” Shorn Arwa aliandika.

Aliwaambia mashabiki wake kwamba kuna faida nyingi kutoka kwa kununua kitabu chake ili kufaidi makubwa lakini hawataki huku akiwaonyesha makubwa ambayo amejizolea kutokana na kuwa mhamasishaji wa bidhaa za nywele.

“Kila siku nawaambia nunua kitabu changu ili kuwa influencer wa wigi hamtaki, angalia baadhi ya vifurushi vya mawigi ambavyo nimepokea, sikuwa hapa, nilikuwa kijijini. Angalia vitu ambavyo nimepokea, nunua kitabu changu uwe influencer wa wigi, hamsikii,” Arwa alisema huku akipanga zawadi zake.