“Fufua Mr Ibu basi!” Wanaijeria wamjia juu pasta aliyedai kufufua watu 50 kwa mwaka (video)

Chris Oyakhilome alibainisha kuwa watu hawa zaidi ya 50 anaowafufua ni mchanganyiko wa wazee na vijana kutoka nchi mbalimbali.

Muhtasari

• Akitoa mwanga zaidi kuhusu hilo, Chris Oyakhilome alikemea kuwa kuna baadhi ya visa ambapo aliwalea watu walioaga hospitalini.

Pastor Chris Oyakhilome
Pastor Chris Oyakhilome
Image: Facebook

Watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii nchini Nigeria wamemjia juu Mchungaji maarufu kwa jina Chris Oyakhilome baada ya mtu wa Mungu kujivunia kuwarudisha hai zaidi ya watu 50 kutoka kifo.

Katika video hiyo, Chris Oyakhilome, mchungaji mwanzilishi wa Kanisa la Mega Christ Embassy anasema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, amefufua zaidi ya watu hamsini kutoka wafu na kuwa hai.

Chris Oyakhilome alibainisha kuwa watu hawa zaidi ya 50 anaowafufua ni mchanganyiko wa wazee na vijana kutoka nchi mbalimbali.

Akitoa mwanga zaidi kuhusu hilo, Chris Oyakhilome alikemea kuwa kuna baadhi ya visa ambapo aliwalea watu walioaga hospitalini.

Baada ya mchungaji Chris Oyakhilome kujivunia kuwafufua zaidi ya watu 50 kutoka kwa kifo kuwafufua, watu walimtaka kujibu kwa kurejesha hai baadhi ya watu maarufu ambao wamefariki dunia.

MMoja kwa jina Daddy Freeze anayetajwa kuwa mwanahabari maarufu nchini humo alimtaka mchungaji huyo kufanya mfano hai kwa kuanza na msanii Mohbad aliyefariki mwaka jana kwa njia tatanisha na kifa kumfufua pia muigizaji maarufu Mr Ibu aliyefariki wiki chache zilizopita.

Daddy Freeze aliandika; "Mungu akubariki sana bwana, tafadhali unaweza kuongeza Mohbad na Mr Ibu kwenye orodha asante kwa kutarajia msaada wako."

Tazama video ya mtumishi wa Mungu akidai kuwafufua wafu hapa;