Mpenzi wa zamani wa YouTuber Mungai Ever, Director Trevor amedokeza kurudi sokoni kutafuta mrithi wa Eve katika moyo wake.
Akizungumza na waandishi wa bahari za burudani, Trevor alichukua fursa hiyo na kutaja baadhi ya vigezo na sifa ambazo atakuwa anazinagalia kwa mpenzi mpya kabla ya kumpitisha kuwa mpenzi wake.
Trevor alijibu sifa anazopenda katika mwanamke akitoa maelezo ya kile mpenzi wake ajae anapaswa kuwa nao katika suala la urembo wa kimwili.
Trevor alichora taswira ya mrembo anayemuona kwenye fikira zake na kusema kwamba ni lazima awe mweupe, mrefu kidogo lakini pia mwenye akili.
“Ngozi nyepesi kidogo, mrefu lakini asinizidi urefu. Awe na Mwili umeboreshwa; maziwa kidogo na pale nyuma pia awe ameumbika vizuri,” alisema.
Trevor pia alifichua angetaka rafiki wa kike mwenye akili. Alisema kuwa mbali na sura ya mwili mwanamke huyo anapaswa kuwa na akili timamu.
“Akili nayo lazima pia akuwe nayo.”
Alitengana na mpenzi wake wa muda mrefu Mungai Eve mwezi mmoja uliopita na huenda akawa anatazamia kurudi kwenye uchumba tena huku akieleza kile anachopenda katika siku zijazo.
Trevor na Mungai Eve waliishi maisha ya kutamanika na kuwafanya wengi kuwaona kama wanandoa wa nguvu na kuwaacha mashabiki wao wakiwa na wivu walipokuwa wakitaniana na kudhihirisha mapenzi yao mtandaoni.
Hata hivyo, penzi lilifika mwisho, likajaa na kupwa kabla ya kuanza kutupiana lawana, kila mmoja akidai mwenzake ndiye chanzo cha kutengana.