Otile Brown akanusha kutumia mazishi ya Brian Chira ku'clout chase kwa ajili ya albamu yake

“Sio mimi ninafanya chochote, ni watu tu ambao wanasukuma huo wimbo na wakasema niende nionyeshe upendo katika safari yake ya mwisho.”

Muhtasari

• Msanii huyo ambaye alitumbuiza kibao chake cha ‘One Call’ katika mazishi ya Chira alisema kwamba yeye hata hakuwa anajua chochote kuhusu Chira.

Otle Brown
Otle Brown
Image: Maktaba, Screengrab

Msanii Otile Brown amekanusha kutumia kifo cha tiktoker Brian Chira kujilimbikizia takwimu za utitihaji na utazamwaji wa albamu yake mpya ya Grace.

Akizungumza na Kenya Online Media, Otile alisema kwamba yeye alifanya tu kwa kupenda na kumheshimisha Chira katika safari yake ya mwisho duniani, akifichua kwamba hata hakuwa anamjua.

Brown alikuwa msanii mkubwa ambaye alijitolea kutumbuiza bila malipo katika mazishi ya tiktoker huyo ambayo yalifanyika Jumanne nyumbani kwa nyanya yake Githunguri kaunti ya Kiambu.

“Kusema kweli albamu yangu inahusiana kivipi na marehemu? Unajua watu ambao wananijua watakuambia kwamba nilichokionesha si kingine Zaidi na upendo, na mimi sikuwa namjua kijana huyo [Brian Chira] ni jinsi mashabiki walivyonivuta kwa jinsi walivyomuomboleza,” Otile Brown alisema.

Msanii huyo ambaye alitumbuiza kibao chake cha ‘One Call’ katika mazishi ya Chira alisema kwamba yeye hata hakuwa anajua chochote na aliona jinsi mashabiki wengi walivyokuwa wkaimrushia jumbe wakati anafanya mahojiano na blogu moja ya Tanzania.

“Mashabiki walikuwa wananiambia baada ya interview vniimbe huo wimbo, mimi hata sikuwa namjua huyo kijana, sijawahi hata zunguma naye, wala kukutana naye. Lakini baada ya kufanya uchunguzi kidogo kumhusu, nilifahamu kwamba ni shabiki wangu mkubwa,” Otile alisema.

Akizungumzia wimbo huo ambao umepata utazamwaji mkubwa baada ya kifo cha Chira, Oitle alisema kwamba wengi walihusisha wimbo wa ‘One Call’ na Chira na hata sasa comment nyingi ni kumhusu marehemu.

“Sio mimi ninafanya chochote, ni watu tu ambao wanasukuma huo wimbo na wakasema niende nionyeshe upendo katika safari yake ya mwisho.”