Simon Kabu kuwapeleka Baba Talisha na nyanyake Brian Chira likizo ya siku 3 na usiku 2 Diani

Simon Kabu alisema kampuni yake itawafadhili wawili hao kwa safari ya angani kwenda Diani kufurahia likizo ya siku tatu na usiku 2.

Muhtasari

• Awali, wanamitandao walimuomba Baba Talisha kuendelea kumshika mkono nyanya huyo baada ya kusimama naye katika kipindi cha wiki mbali tangia mjukuu wake alipofariki.

Baba Talisha na nyanyake Chira.
Baba Talisha na nyanyake Chira.
Image: Instagram

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya kusafirisha watalii ya Bonfire Adventures, Simon Kabu ameonesha kuguswa na jinsi tiktoker Baba Talisha alivyojifunga kibwebwe na kuwa kwenye mstari wa mbele kuongoza na kufanikisha mazishi ya Brian Chira.

Kabu kupitia ukurasa wake wa Instagram, alisema kwamba kutokana na kuguswa huko, kampuni yake ya Bonfire Adventures imeamua kumtunuku Baba Talisha na nyanyake Chira likiza ya siku tatu na usiku 2 kujivinjari katika fukwe za Diani kaunti ya Kwale.

Kabu alisema kwamba ni wawili hao sasa kukubali na kuchagua siku ambazo watakuwa wanataka kwenda kutumikia likizo yao ya kujivinjari Diani.

“Baba Talisha … na Shosho ya Chira. Nadhani baadhi ya juhudi zinastahili kutambuliwa. BONFIRE ADVENTURES imewalipia siku 3 usiku 2 Likizo ya kwa nijia ya ndege kwenda Diani kwa wakati muupendao,” alisema.

Baba Talisha na nyanyake Brian Chira walisimama kidete na kuona michango ikifika hadi milioni 8 mitandaoni iliyokusudiwa kuendesha shughuli zote za mazishi na zingine zisalie kumsaidia mkongwe huyo.

Awali, wanamitandao walimuomba Baba Talisha kuendelea kumshika mkono nyanya huyo baada ya kusimama naye katika kipindi cha wiki mbali tangia mjukuu wake alipofariki.