Dem wa FB afichua idadi ya nguo ambazo alipatiwa na mkewe Mulamwah, Ruth K

Wakati Ruth K alikuwa anamkabidhi Dem wa FB nguo hizo, Ruth K alisema kwamba zilikuwa hazimtoshi kutokana na kuongeza mwili baada ya mimba na kujifungua

Muhtasari

• Alisema kwamba alijipima nguo 15 laini mwisho wa siku nguo ambazo aliondoka nazo kwenda kwake ni nguo 3 tu na ambazo hawezi kuzivaa kwa sasa.

Dem wa FB
Dem wa FB
Image: Screengrab//YT

Mchekeshaji chipukizi, Dem wa Facebook amefunguka ukweli kuhusu video ambayo alionekana nyumbani kwa Mulamwah akipokezwa rundo la nguo na Ruth K.

Katika mazungumzo na Obinna, Dem wa FB alisema kwamba japo kilikuwa kipindi, lakini hakuenda nyumbani na rundo la nguo zote ambazo alionekana akizipokea kutoka kwa Ruth K katika sebule ya makazi yao mapya na Mulamwah.

Alisema kwamba alijipima nguo 15 laini mwisho wa siku nguo ambazo aliondoka nazo kwenda kwake ni nguo 3 tu na ambazo hawezi kuzivaa kwa sasa.

“Sikuomba nguo, si ningekuwa nimezivaa kama kweli niliomba. Ilikuwa ni kipindi kidogo lakini hata hivyo nilienda nyumbani na nguo 3 hivi lakini siwezi nikazivaa sasa hivi kwa sababu nikivaa watu wataanza kusema ni ya Bibi wa Mulamwah hata ile yangu nimenunua Gikomba,” alisema.

“Nilijipima nguo 15 na akasema amenipa 15 lakini behind the scenes nilienda nyumbani na nguo 3. Sasa hivi kila mtu ananiambia nivae hizo nguo za Ruth K hadi nashangaa ni nguo gani,” mrembo huyo alisema.

Hata hivyo, Dem wa FB alishukuru kwa zawadi ya nguo lakini akawataka watu wasiseme kwamba kila nguo anayovaa sasa hivi ni ya Ruth K.

Wiki iliyopita, Ruth K kupitia ukurasa wake wa YouTube alichapisha video wakiwa na Dem wa FB katika makazi yao mapya kabla ya kuingia chumbani na kuonekana akimpa zawadi ya nguo.

Wakati wa kumkabidhi nguo hizo, Ruth K alisema kwamba zilikuwa hazimtoshi kutokana na kuongeza mwili baada ya mimba na kujifungua.