Harmonize na Baba Levo wakutana na kusameheana wiki kadhaa baada ya kuzika tofauti na Diamond

Baba Levo na Harmonize wanakutana na kuzika tofauti zao, ikiwa ni wiki chache tu baada ya Harmonize kukutana na kusalimiana na Diamond Platnumz, baada ya Zaidi ya miaka 4 bila kuonana.

Muhtasari

• Hata hivyo, Harmonize hakuwahi kulizungumzia hilo licha ya Baba Levo kudai kwamba alikuwa anasubiri kupona ili kumburura Harmonize mahakamani kwa kumshambulia.

BABA LEVO NA HARMONIZE WASAMEHEANA
BABA LEVO NA HARMONIZE WASAMEHEANA
Image: instagram

Hatmaye Harmonize na chawa wa WCB Wasafi, Baba Levo wamekutana na kuzika tofuati zao, baada ya wiki kadhaa za sakata la Harmonize kutuhumiwa kumshambulia mtangazaji huyo wa Wasafi.

Wawili hao walikutanishwa na jamaa mmoja kwa jina Joseph Kusaga na kwenye video ambayo wote wawili kila mmoja ameichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, walikutanishwa na kupeana mikono ishara ya kuzika uhasama.

Harmonzie aliinukuu video hiyo kwamba ‘amani lazima itangazwe’ huku Baba Levo akinukuu video kwa ukurasa wake kwamba ‘Neno samahani lina maana kubwa sana kwenye maisha yangu …!!! Kwa busara za mzee @josephkusaga 🙏🙏 nimekusamehe mdogo wangu Harmonize.”

Awali, Baba Levo katika msururu wa mahojiano alisema alishambuliwa na Harmonize na kumbindua shingo akidai kwamba zogo lao lilitokea katika kumbi moja ya kucheza bahati nasibu.

Baba Levo alidai kwamba tajiri mmoja aliwakabidhi pesa wagawanye, akiwemo Harmonize lakini msanii huyo wa Konde Gang akachukua mgao mkubwa jambo ambalo lilimpelekea yeye kumkabili kutaja kujua kwa nini alifanya hivyo lakini akajibiwa kwa kukunjwa mashati.

Hata hivyo, Harmonize hakuwahi kulizungumzia hilo licha ya Baba Levo kudai kwamba alikuwa anasubiri kupona ili kumburura Harmonize mahakamani kwa kumshambulia.

Lakini pia kando na zogo hilo la madai, Harmonize kwa muda mrefu amekuwa akimpuuzilia mbali Baba Levo kwa kile anasema analipwa na Diamond ili kumchafulia jina.

Baba Levo na Harmonize wanakutana na kuzika tofauti zao, ikiwa ni wiki chache tu baada ya Harmonize kukutana na kusalimiana na Diamond Platnumz, baada ya Zaidi ya miaka 4 bila kuonana.