Uko sure tukipatana na chali yako nikiwa na Harrier hataingia box? – Kinuthia awauliza warembo

Crossdresser huyo aliashiria kwamba hakuna mwanamume yeyote anayeweza kumkataa endapo ataamua kuwafuata na kuwatongoza, na haswa wakiona kwamba ako na gari aina ya Harrier.

Muhtasari

• Kinuthia amekuwa akigonga vichwa vya habari tangu ujio wa TikTok humu nchini takribani miaka 3 iliyopita.

KINUTHIA
KINUTHIA
Image: instagram

TikToker maarufu kwa kuvaa mavazi kinyume na jinsia yake, Kelvin Kinuthia amewapa changamoto warembo kuhusu wapenzi wao wa sasa.

Kupitia Instagram, Kinuthia alipakia video akiwa ndani ya nyumba na kuandika kwenye video hiyo swali lake kwa warembo.

Kinuthia aliwauliza warembo wanaomfuatilia kama wako na uhakika akiamua kuwataka wapenzi wao wa kiume watamkataa.

Crossdresser huyo aliashiria kwamba hakuna mwanamume yeyote anayeweza kumkataa endapo ataamua kuwafuata na kuwatongoza, na haswa wakiona kwamba ako na gari aina ya Harrier, moja kwa moja kila mwanamume atamkubalia bila kuangalia nyuma.

“Hata wewe ukiangalia, tukipatana na chali yako nikiwa na Harrier, uko na uhakika hataingia kwenye box yangu?” Kinuthia aliuliza.

Kinuthia amekuwa akigonga vichwa vya habari tangu ujio wa TikTok humu nchini takribani miaka 3 iliyopita.

Kijana huyo ambaye amejitengenezea jina na wasifu kama mwanamke amekuwa akitoa changamoto na kuwakosesha usingizi baadhi ya warembo ambao anadai hawawezi kumfikia kwa mavazi na hata kwa kujipodoa.

Mwanzoni kabla watu hawajamzoea, Kinuthia alikuwa anakumbwa na maswali mengi kutoka kwa wanamitandao, baadhi wakitaka kujua msimamo wake kijinsia.

Hata hivyo, Kinuthia hakuwahi kuweka wasi msimamo wake wa kijinsia, hivyo kuwaacha wengi katika hali ya kubahatisha na wengine moja kwa moja kumweka kwenye mrengo wa wapenzi wa jinsia moja.